BONDIA Lennox Lewis amewaambia mapromota wa Urusi atarejea kupigana na mmoja kati ya ndugu akina Klitschko kwa dau kubwa zaidi katka historia ya ndondi za kulipwa.
Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 48, ambaye bado ni bingwa zaidi asiyepingika, alipewa ofa ya dola z Kimarekani Milioni 50 (Pauni Milioni 31.3) mjini Moscow mwishoni mwa wiki, alipokwenda kutazama pambano la Wladimir Klitschko akitetea mataji yake ya dunia dhidi ya Alexander Povetkin.
Lewis alijibu kwa kuahidi kurejea ulingoni kwa dau la dola za Kimarekani Milioni 100 (Pauni Milioni 62.6).
Mapromota wanatafakari kuongeza dau mara mbili na Lewis amesema: "Hiyo ndiyo bei yangu nayotaka na ipo chini ya mjadala. Nimewaambia ninaweza kuwa tayari ndani ya miezi sita na nipo katika mazoezi ya kawaida,".
Kurejea: Lennox Lewis amesema atapigana na mmoja kati ya ndugu akina Klitschko (chini) kwa dola za Kimarekani Milioni 100
Ndugu wapiganaji: Wladimir (kushoto) alitetea mataji yake ya dunia Jumamosi wakati Vitali amekuwa akijishughulisha na siasa
Lewis, yupo London kuanzisha akademi yake mpya ya mazoezi kuandaa mabingwa wa dunia wa uzito wa juu wa baadaye, anakimbia kila siku asubuhi Hyde Park.
Amesema yuko fiti kabisa akiwa na uzito wa Pauni 245. Lewis anaamini katika pambano lijalo anaweza akarudia yaliyofanywa na George Foreman, ambaye alirejea ulingoni na kutwaa ubingwa wa dunia akiwa na umri wa miaka 48, akiwa anashikilia rekodi ya bondia 'babu' zaidi kuwahi kutwaa taji la uzito wa juu kihistoria.
Bei anayotaka kwa pambano lake lijalo akitoka kustaafu, inaweza kumfanya aweke rekodi ya kuwa bondia aliyewahi kulipwa fedha nyingi zaidi katika historia ya masumbwi.
Mkali wa kutupa mikono: Lewis alimpiga Vitali wakati pambano liliposimamishwa raundi ya sita baadya kumchana vibaya mpinzani wake huyo
Unaikumbuka hii?: Klitschko alikuwa anaongoza kwa pointi za majaji wote watatu wakati pambano linasimamishwa- mara ya mwisho alipopigana na Lewis
Floyd Mayweather anashikilia rekodi ya ya kulipwa fedha nyingi, ambazo ni dola za Kimarekani Milioni 41.2 alizolipwa katika pambano lake la mwezi uliopita na bondia wa Mexico, Canelo Alvarez, na dau lake linatarajiwa kupanda hadi dola Milioni 70 baada ya malipo yote.
Awali, Lewis alisema anaweza kurejea ulingoni kwa dola Milioni 50, lakini sasa anasema; "Nilisema wakati huo Dola Milioni 50 zingetosha kuvua pajama langu, lakini sasa napaswa kutafakari thamani ya heshima yangu kustaafu kama bingwa asiyepingika. Hiyo itawagharimu dola zKImarekani Milioni 100,".
Chali na kwisha kazi: Wladimir Klitschko alimdondosha Alexander Povetkin mara nne na kutetea mataji yake ya dunia
'VIBABU' VILIVYOFANYA MIUJIZA ULINGONI
George Foreman — Baada ya muongo mmoja wa kuwa nje ya ulingno, alirejea katika umri wa miaka 38 na kupigana kwa miaka mingine 10. Alitwaa tena mataji ya dunia ya IBF na WBA aliyoyapoteza kwa Muhammad Ali miaka 20 iliyotangulia kwa kumpiga Michael Moorer mwaka 1994 (chini).
Evander Holyfield — Alistaafu mwaka 1994 kutokana na matatizo ya moyo, lakini akarejea baada ya kufanyiwa maombi na akapigana na Brian Nielsen mwaka 2011.
Riddick Bowe — Alistaafu akiwa na umri wa miaka 28 kujiunga na jeshi la wana maji la Marekani, lakini akakimbia baada ya siku tatu za mafunzo na kurejea ulingoni mia saba baadaye. Pambano lake la mwisho lilikuwa mwaka 2008, akiwa na umri wa miaka 41.
Ricky Hatton — Alistaafu baada ya kupigwa na Floyd Mayweather mwaka 2007 na Manny Pacquiao mwaka 2009, lakini akarejea mwaka 2012 kupambana na Vyacheslav Senchenko, ambaye alimsimamisha katika raundi ya nane (chini).
Sugar Ray Leonard — Alistaafu mara nne kuanzia mwaka 1982 na 1997.
Zingatia: Bernard Hopkins atatetea taji la uzito wa Light-heavy mwezi huu akiwa na umri wa miaka 48 na miezi tisa
0 comments:
Post a Comment