// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KUELEKEA PAMBANO LA WATANI JUMAPILI; KWELI SIMBA SC NI YA MAKINDA WASIO NA UZOEFU? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KUELEKEA PAMBANO LA WATANI JUMAPILI; KWELI SIMBA SC NI YA MAKINDA WASIO NA UZOEFU? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 16, 2013

    KUELEKEA PAMBANO LA WATANI JUMAPILI; KWELI SIMBA SC NI YA MAKINDA WASIO NA UZOEFU?

    Na mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam 
    NYASI za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumapili zinatarajiwa kuwaka moto kwa mpambano wa watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. BIN ZUBEIRY inaanza kukuletea mfululizo wa makala za kuelekea pambano hilo linalobeba picha halisi ya soka ya Tanzania na leo tunaangalia kikosi cha Simba SC, kweli wachezaji wake ni wachanga hawawezi kuhimilii vishindo vya mechi ya watani Jumapili? Endelea.
    Hawa ni watoto? Kikosi cha Simba SC kutoka kulia Amri Kiemba, Kaze Gilbert, Amisi Tambwe, Betram Mombeki, Haroun Chanongo, Joseph Owino, Issa Rashid 'Baba Ubaya', Jonas Mkude, William Lucian 'Gallas' na Twaha Shekuwe 'Messi'. Ni kikosi cha uwiano mzuri.  

    WATU wanasema kikosi cha Simba kinaundwa na wachezaji wenye umri mdogo, wasio na uzoefu waliopandishwa kutoka kikosi cha vijana na kwa sababu hiyo, Yanga yenye kikosi kizima cha wachezaji wazoefu inapewa nafasi ya kushinda Jumapili.
    Lakini ukirejea kikosi cha kwanza cha Simba, unagundua huo si kweli- bali katika kikosi cha Simba kuna damu changa kadhaa zilizoonyesha uwezo mkubwa kiasi cha kuaminiwa, hadi baadhi ya wachezaji ‘mafaza’ wakawekwa kando kama akina Haruna Moshi ‘Boban’, Juma Nyosso, Amir Maftah na wengineo.
    Ni wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao wameudhihirisha katika mechi za Ligi Kuu walizocheza, kiasi cha wengine kuitwa hadi timu ya taifa, Taifa Stars kuanzia mwaka juzi kama Haruna Chanongo, Edward Christopher na Jonas Mkude.
    Betram Mombeki ni mpiganaji

    Kikosi cha Simba ambacho kimekuwa kikicheza siku za karibuni ni; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte anatarajiwa kuchukua nafasi ya majeruhi Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Gilbert Kaze, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ anaweza kucheza badala ya Said Ndemla, Betram Mombeki, Amisi Tambwe na Haroun Chanongo. 
    Au kocha Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ anaweza kumuanzisha yeyote kati ya Andrew Ntalla, William Lucian ‘Gallas’, Hassan Hatibu, Rashid Ismail, Sino Augustino, Ramadhani Singano ‘Messi’, Edward Christopher, Zahor Pazi, Twaha Shekuwe ‘Messi’ badala ya wanatarajiwa hapo juu. 
    Kwa ujumla Simba SC ni timu yenye uwiano mzuri na ndiyo maana imefanikiwa kuongoza Ligi Kuu hadi sasa, baada ya kujikusanyia pointi 19 katika mechi nane, ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi, Yanga SC.
    Tambwe Amisi ni fundi, anajua kufunga

    Ina wachezaji wenye uwezo mkubwa kuanzia safu ya ulinzi, kiungo hadi ushambuliaji na ndiyo timu ambayo inatoa mchezaji anayeongoza kwa mabao katika Ligi Kuu, Mrundi Amisi Tambwe mwenye mabao nane hadi sasa, ambao ni wastani wa bao moja kila mechi.  
    Ina viungo hatari wa pembeni akina Chanongo, Twaha, Singano na Sino Augustino ambao kati watakaopangwa wanaweza kuwapikia mabao washambuliaji Tambwe na Mombeki. Pale mbele, Mombeki ni mchezaji mpiganaji uwanjani na Tambwe ni mtu wa mipango- maana yake unaweza kuiona shughuli ambayo itawakabili mabeki wa Yanga Jumapili. Mtaalamu Amri Kiemba huwa anachezeshwa kama mchezaji huru kwa sababu ni fundi sana na ndiye amekuwa akifunga mabao ya Simba katika mechi dhidi ya watani siku za karibuni. 
    Kaze Gilbert ni bonge la beki

    Kwa Yanga, ukuta unajulikana, Ally Mustafa ‘Barthez’ atakuwa analindwa na Mbuyu Twite  kulia, kushoto David Luhende kulia, katikati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan, wakati kiungo mkabaji atakuwa mtu mzima, Athumani Iddi ‘Chuji’.
    Mbele, kulia atakuwa anateleza Mrisho Ngassa, kushoto Haruna Niyonzima katikati Frank Domayo na washambuliaji wanaweza kuanza Didier Kavumbangu na Hamisi Kiiza. 
    Kocha Mholanzi, Ernie Brandts bado anaweza kuamua kufanya mabadiliko katika kikosi kitarajiwa kwa kumuingiza yeyote kati ya Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Salum Telela, Said Bahanuzi, Hussein Javu, Jerry Tegete na Abdallah Mguhi.
    Kwa tathmini halisi ya vikosi vya timu zote kama makocha wataziandaa vyema timu zao na kupanga vyema timu, mechi itakuwa kali na nzuri na tofauti na inavyodhaniwa kwamba itakuwa ya upande ya mmoja, kwa madai Simba SC ina watoto wengi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUELEKEA PAMBANO LA WATANI JUMAPILI; KWELI SIMBA SC NI YA MAKINDA WASIO NA UZOEFU? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top