KOCHA Carlo Ancelotti hajaamua kama atamuanzisha Gareth Bale katika mechi ya El Clasico kesho, lakini amesema nyota huyo wa Wales yupo tayari.
Mtaliano huyo, akizungumza katika Mkutano wa Real Madrid na Waandishi wa Habari leo mchana amesema kwamba maamuzi yoyote kuhusu Bale atayafanya baada ya mazoezi ya mwisho kuelekea mechi hiyo jioni ya leo kabla ya mechi na Barcelona Uwanja wa Camp Nou Jumamosi jioni.
Ancelotti alisema; "Ikiwa kutakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari baada ya mazoezi ya jioni, nitawaambia vizuri kuhusu Bale kama ataanza,".
Kocha wa Real, Carlo Ancelotti amethitisha Bale (juu) yuko tayari kuanza
Waliotokea Spurs: Bale akipasha misuli moto kwa pamoja na mchezaji mwenzake wa zaani wa Tottenham, Luka Modric (kulia)
Walini noma: Bale atatumai kuanza pamoja na Cristiano Ronaldo katika El Clasico
Watu fedha: Wachezaji ghali duniani, Bale (kushoto) na Ronaldo (kulia)
uamuzi mwishoni: Ancelotti ataangali kama anaweza kumuanzisha Bale katika mechi kubwa
Siku ya mazoezi: Wachezaji Real Madrid wakijifua
Kwa raha zao: Xabi Alonso (kushoto) na Isco (kulia) wakitaniana wakati wa mazoezi
Baada ya kubanwa sana kwa maswali juu ya suala hilo, Ancelotti alisema kwamba Bale yuko tayari na hayuko katika wakati mgumu tena, lakini amejtuma sana na ametumia mapumziko ya mechi za kimataifa kujiweka fiti.'
"Kwa maoni yangu, na maoni yake pia, yuko tayari kucheza tangu mwanzo,"alisema.
Bale hajawa na mwanzo mzuri Real kutokana na kuandamwa na majeruhi tangu ajiunge na klabu hiyo ya Hispania. Kwa ujumla, mwanasoka huyo wa kimataifa wa Wales amecheza dakika 178 tu katika mechi tano na kufunga bao moja.
Juve imemrudisha: Bale alicheza katikati ya wki dhidi ya Juventus
0 comments:
Post a Comment