ALIZALIWA kama Cassius Clay, lakini anafahamika zaidi kwa jina Kiislamu alilochagua, Muhammad Ali.
Wakati kuna picha nyingi zikimuonyesha gwiji huyo wa ngumi akiwa ulingoni, ni picha chache sana zinamuonyesha katika miaka ambayo alifungiwa katika mchezo huo kwa kugoma kuingia jeshini kupigana vita dhidi ya Vietnam.
"Vita ni kinyume cha mafundisho ya Qur'an tukufu,"alisema. "Siwezi kujaribu kukikuka maandiko. Haturuhusiwi kuingia kwenye vita isipokuwa tu mwa maelekezo yake Allah au Mitume wake. Hatuiingii kwenye vita na Wakristo au yeyote asiyeamini,".
Alipogoma kufanya hivyo Aprili 28, mwaka 1967, si kwamba alikamatwa tu, bali alipokonywa leseni ya ngumi na kuvumuliwa mataji yote.
Baadaye Mahakama ya Houston, Texas ilimkuta na hatia, alkini Mahakama Kuu ya Marekani ilifuta maamuzi hayo mwaka 1971 na Ali akawa huru kurejea ulingoni tena.
Ali hakutumikia kifungo jela, lakini alizuiwa kupiana kati ya mwaka 1967 na 1971.
Wakati amezuiwa kupigana alitumia muda wake kuzungumzia masuala ya haki katika shule na vyuo vikuu.
"Nina furaha kwa sababu nipo huru," alisema akizungumza na jarida la Time mwaka 1968. "Nimeweka msimamo ambao watu weusi wote watauchukua muda si mrefu,"alisema.
Zifuatazo ni picha zinazomuonyesha Ali kati ya tangu 1968, wakati bondia huyo alipofungiwa, lakini akaendelea kuteka hisia za Wamarekani nchini humo.
Magwiji walipokutana: Ali (kulia) akizungumza na James Earl Jones (kushoto) ambaye alishinda tuzo ya Tony kama mwigizaji bora Best katika picha ya The Great White Hope mwaka 1969
Ali akiwa amesimama katika picha iliyochukuliwa kwenye sinema ya The Great White Hope alipohudhuria onyesho la sinema hiyo
Ali akitaniana na rafiki
Ali akizungumza na umati wa wanafunzi 1,500 mjini Los Angeles Februari, mwaka 1968.
Utata: Ali akizungumza na Waandishi wa Habari UCLA
Ali alikuwepo katika ukumbi wa San Francisco City Aprili 27, mwaka 1968. Lakini hotuba yake ilizuia kizaazaa mbele ya watu 12,500 alipozungumzia Waislamu weusi
Nyumbani kwake Chicago, Ali akiwa amepigwa picha anasoma kitabu cha 'Message to the Black Man' kilichoandikwa na Elihad Muhammad, kiongozi wa Waislamu wa taifa hilo
Ali akisalimia wanafunzi wa St John's University huko Queens, New York Mei mwaka 1968
Jicho la Chui: Muhammad Ali akiangalia picha ya bondia Sonny LIston ambaye alikuwa anajiandaa kupambana naye wakati huo
Siku ya Uhuru: Bondia huyo alihudhuria chakula cha usiku kwa heshima ya Floyd McKissick (wa pili kushoto), huko Columbus, Ohio Julai 4, mwaka 1968.
0 comments:
Post a Comment