WASHAMBULIAJI Didier Drogba, Salomon Kalou na Gervinho wote wamefunga leo Ivory Coast ikiifumua 3-1 Senegal na kuongeza matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Drogba alifunga kwa penalti dakika ya tano, kabla ya winga wa zamani wa Arsenal, Gervinho kufunga la pili dakika tisa na baadaye kipindi cha pili Salomon Kalou akafunga la tatu mjini Abidjan.
Bao pekee la Senegal lilifungwa na Papiss Cisse dakika tano kabla ya filimbi ya mwisho.
Tembo wauwaji: Wachezaji wa Ivory Coast wakishangilia ushindi wao leo
Sasa Ivory Coast watahitaji sare au kufungwa si zaidi ya wastani wa bao moja katika mchezo wa marudiano moja ili kujikatia tiketi ya Brazil mwakani. Seneal yenyewe itahitaji kushinda 2-0 tu nyumbani, ili kujihakikishia kurejea Fainali za Kombe la Dunia.
Didier Drogba ameifungia Ivory Coast leo
Salomon Kalou na Drogba walicheza pamoja Chelsea miaka kadhaa
Umefanya vizuri: Gervinho akizungumza na kocha Sabri Lamouchi baada ya mechi
0 comments:
Post a Comment