RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amesema kwamba mapato ya klabu yake tajiri zaidi duniani yanaweza kumnunua mshambuliaji wa Monaco, raia Colombia, Radamel Falcao mwakani.
Akizungumza katika chati ya shoo ya soka, Punto Pelota jana usiku, Perez alitolea nje uwezekano wa usajili wa Falcao katika dirisha dogo Januari, lakini akasema Real lazima iwe karibu naye mwishoni mwa msimu.
Falcao, mwenye umri wa miaka 27, aliondoka kwa wapinzani wa Jiji wa Real, Atletico kwenda kujiunga na Monaco mwishoni mwa msimu uliopita kwa dau lililoripotiwa kuwa kiasi cha Pauni Milioni 53.
Madrid return: Real president Florentino Perez has hinted they could bid for Monaco and Colombia striker Radamel Falcao next summer
Tuko njiani: Falcao akipiga penalti alipoichezea Colombia mechi ya kufuzu Kombe la Dunia na Chile mjini Barranquilla Ijumaa timu hizo zikitoka sare ya 3-3.
"Yeye (Falcao) hatakuja Januari, lakini Juni, nani anafahamu?"alihoji Perez. "Hakuna kisichowezekana na kuna muda wa kutosha kutoka sasa hadi huko.
"Falcao ni mchezaji mkubwa na ninajua anataka kucheza (Real) Madrid. Ninatambua hilo, lakini ni kawaida. Wameniambia,".
Mipango kamambe: Rais wa Real, Florentino Perez akiwa mchezaji ghali duniani aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86, Gareth Bale. Sasa anataka Falcao awe Galactico mpya
Yuko juu: Mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 53, Falcao tayari ameifungia mabao saba katika klabu yake mpya, Monaco msimu huu
Sababu moja kubwa Real kuingia sokoni kusaka mshambuliaji ni kushuka kwa kiwango cha mshambuliaji wake Mfaransa, Karim Benzema.
Kipenzi hicho cha Perez, Benzema ameshindwa kuteka hisia za mashabiki wa Real tangu awasili mwaka 2009 na hana furaha sana mbele ya umati wa Bernabeu.
Perez amekuwa akimtetea mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa akilaumiwa na kocha wa Real, Carlo Ancelotti kwa kutojituma kiasi cha kutosha uwanjani.
Hali tete: Mshambuliaji Karim Benzema amekuwa akikandiwa na mashabiki Uwanja wa Bernabeu na kocha wake, Carlo Ancelotti chini anamlaumu kwa kutojituma kiasi cha kustosha uwanjani
0 comments:
Post a Comment