NI sawa kusema kiungo wa Chile, Arturo Vidal hakuwa na usiku mzuri jana.
Vidal alikuwa sehemu ya kikosi cha Juventus kilichoendelea na mwanzo mbaya mbaya wa msimu huu baada ya kufungwa 2-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Real Madrid.
Na pamoja na hayo, alifanya kituko cha kijinganga sana yeye mwenyewe binafsi kusaka penalti rahisi, baada ya kujirusha kwenye eneo la hatari bila hata kuguswa.
Vidal alipoteza mpira yeye mwenyewe akiwa ameingia kwenye eneo la hatari la Real na kupiga nyasi hivyo mpira ukapoteza mwelekeo, naye akajirusha chini kwenye nyasi za Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Wakati mpira unavuka mstari kutoka nje ili ipigwe goal-kick, huku kukiwa hakuna beki jirani naye, Vidal alianza kulalamika kumuomba refa atoe penalti akiwa ameanguka chini.
Kuyapa uzito madai yake akanyoosha kidole kabisa kumdanganya refa eti amechezewa faulo ba beki wa Madrid aliyekuwa karibu yake. Ni salama kusema alikuwa analetra umagumashi.
Bahati mbaya: Vidal alipiga nyasi badala ya mpira huku kukiwa hakuna beki wa Real jirani naye
Aliingia vizuri tu: Kiungo huyo wa Chile alifanikiwa kuingia vizuri kwenye eneo la hatari la Real
Abaruka: Vidal akijirusha
Anajirusha: Kiungo wa Juve akijiandaa kudondokea kwenye nyasi baada ya kujirusha
Una uhakika? Wachezaji wa Real wakionekana kuchanganyikiwa wakati Vidal anawanyooshea kidole
Juventus haijainda mechi hadi sasa katika Ligi ya Mabingwa msimu huu na inashika nafasi ya tatu katika Kundi B michano hiyo ikiwa imefikia katikati hayua ya makundi, ikizidiwa pointi mbili na Galatasaray wanaoshika nafasi ya pili.
Ushindi wa vinara wa kundi hilo, Madrid umetokana na mabao ya Cristiano Ronaldo mawili, huku Fernando Llorente akifunga bao pekee la Juve.
Hakuna kujirusha! BIN ZUBEIRY inaunga mkono kampeni za Sportsmail kuwazuia wachezaji kudanganya marefa
0 comments:
Post a Comment