TIMU ya taifa ya Ghana imeifunga Misri mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Mshambuliaji Asamoah Gyan alifunga mabao mawili dakika ya tano na 52, wakati Wael Gomaa alijifunga dakika ya 21.
Amefunga: Asamoah Gyan ameifungia Ghana mabao mawili
Mohamed Aboutrika aliifungia bao pekee Misri kwa penalti dakika ya 41, kabla ya Majeed Waris kuifungia Ghana dakika ya 44, Sulley Muntari akafunga kwa penalti dakika ya 72 na mchezaji mpya wa Chelsea, Christian Atsu akahitimisha karamu ya mabao ya Ghana dakika ya 87.
Kikosi cha kilikuwa; Ghana: Dauda, Inkoom, Akaminko, Sumaila, Opare, Essien, Muntari/Badu dk83, K Asamoah, A Ayew/Atsu dk83, Waris, Gyan/Wakasu dk79.
Misri: Ekrami/El Shenawy dk57, A Fathi, W Gomaa, Nagieb, Shedid/Shikibala dk46, Ashour/Mehamadi dk40, Ghaly, El Neny, Aboutrika, W Soliman na M Salah.
0 comments:
Post a Comment