BALAA la majeruhi limezidi kumuandama mchezaji ghali duniani, Gareth Bale katika maisha yake mapya katika klabu ya Real Madrid, baada ya kugundulika anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa ngiri.
Lakini majeruhi hayo hayatarajiwi kuathiri matarajio yake ya kurejea kwake uwanjani kuwahi mechi kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus Oktoba 23 na dhidi ya Barcelona siku tatu baadaye.
Benchi: Bale anaweza kuhitaji upasuaji wa ngiri
Lakini majeruhi hayo hayatarajiwi kumchelewesha kurejea uwanjani kulingana na matarajio yake Oktoba 23
Tatizo hilo ni mbali na matatizo ya misuli yaliyomfanya Bale acheze dakika 132 tu na kuanza katika mechi moja tu msimu huu.
0 comments:
Post a Comment