IMEWEKWA OKTOBA 2, 2013 SAA 1:15 USIKU
MSHAMBULIAJI Samuel Eto'o ambaye Watanzania wanamuita shemeji baada ya kukutwa na skendo ya kutembea na binti mmoja wa Dar es Salaam alipokuja na timu yake ya taifa miaka mitano iyopita, ametumia mshahara wake kununua magari ya kifahari yenye thamani ya jumla ya Pauni Milioni 4.
Gari mpya ya mshambuliaji huyo wa Chelsea ina thamani ya Pauni Milioni 1.55 ambayo ni aina ya Bugatti Veyron ambayo alihamia nayo London pamoja na nyingine tatu akitokea Anzhi msimu huu.
Pamoja na Veyron, Eto'o ametumia Pauni Milioni 1.25 kununua Aston Martin One-77, kwa mujibu wa gazeti la The Sun. Mshambuliaji huyo wa Cameroon mwenye umri wa miaka 31, pia amenunua gari la maraha aina ya Maybach Xenatec kwa Pauni 750,000 na Aston Martin V12 Zagato kwa Pauni 450,000.
Kazini: Samuel Eto'o alitokea benchi na kuisaidia Chelsea kushinda 4-0 dhidi ya Steaua Bucharest
Kitu cha hatari: Eto'o anamiliki Bugatti Veyron kama hii pichani
Si mbaya: Mcameroon huyo pia anamiliki gari la Pauni Milioni 1.25 aina yaAston Martin One-77
Eto'o wakati wote amekuwa mpenzi wa magari na imewahi kuripotiwa alimpa zawadi ya gari mshambuliaji wa zamani wa Cameroon, Roger Milla wakati wa Krisimasi mwaka 2010.
Alisema: "Napenda kuwa na gari chache kwa sababu inanipa nafasi ya kuchagua na haimuumizi yeyote.
"Kuwa mwenye furaha, kitu cha kwanza ni kufurahi na nafsi yako, na nina furaha,".
Kazi nzuri: Eto'o pia anamiliki Maybach Xenatec Coupe yenye thamani ya Pauni 750,000
Na nyingine... Magari ya Eto'o yenye thamani ya jumla ya Pauni Milioni 4 ni pamoja na Aston Martin V12 Zagato, yenye thamani ya Pauni 450,000