WAKATI mechi za kufuzu kwa Fainali Kombe la Dunia zikiwa katika hatua za mwishoni Ulaya, UEFA imewaita baadhi ya wachezaji nyota katika mchezo huo kuwatumia kwa ajili ya kampeni ya kupiga vita ubaguzi wa rangi.
Bodi hiyo ya soka Ulaya imetoa video 32 ikionyesha wachezaji kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo Cristiano Ronaldo, Arjen Robben na Michael Essien wakisaidia kufikisha ujumbe wa UEFA wa kampeni hiyo ya heshima.
Nyota: Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo yumo kwenye video ya UEFA kupiga vita ubaguzi
Essien si mchezaji pekee wa Ligi Kuu ya England aliyeshiriki video hiyo, kwani ameungana na wachezaji wenzake wa The Blues akina Branislav Ivanovic na David Luiz, wakati Manchester City amechukuliwa mchezaji mpya, Stevan Jovetic.
Wawili wa Chelsea: Branislav Ivanovic kushoto ameshiriki video hiyo pamoja na mchezaji mwenzake, Michael Essien
Nyota wa Ligi Kuu England: Beki wa Chelsea, David Luiz na mshambuliaji wa Manchester City, Stevan Jovetic wamo pia
Mwanzo na mwisho: Arjen Robben na Howard Webb pia wamo
0 comments:
Post a Comment