ENGLAND imeongeza matumaini ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kuifumua Montenegro mabao 4-1 usiku huu.
Mabao ya England inayofundishwa na Roy Hodgson yamefungwa na Rooney dakika ya 48, Boskovic akajifunga dakika ya 62, Townsend dakika ya 78 na Sturridge dakika ya 90 kwa penalti, lakini la wageni limefungwa na Damjanovic dakika ya 71.
Kikosi cha England kilikuwa: Hart, Walker, Cahill, Jagielka, Baines, Gerrard/Milner dk87, Lampard/Carrick dk65, Townsend/Wilshere dk80, Rooney, Welbeck na Sturridge
Montenegro: Poleksic, Pavicevic/Beciraj dk57, Kecojevic, Savic, Jovanovic, Zverotic, Drincic, Boskovic, Volkov/Vukcevic dk72, Damjanovic na Jovetic/Kazalica dk81..
Bao safi: Andros Townsend akiifungia England bao la tatu katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa
Shangwe: Townsend akishangilia
Townsend akifanya vitu vyake
Wayne Rooney (Namba 10) akiifunai England bao la kwanza
Leighton Baines akijaribu kupasua ukuta wa Montenegro
Gerrard akipiga juu ya lango
Gerrard akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Branko Boskovic
Presha inapungua: Kocha Roy Hodgson akiangalia vijana Uwanja wa Wembley
Nayo Ujerumani imeendeleza ubabe baada ya kuifumua Jamhuri ya Ireland mabao 3-0 usiku huu, shukrani kwao Khedira aliyefunga dakika ya 12, Schurrle dakika ya 58 na Ozil dakika ya 90.
Sami Khedira akiifungia Ujrumani bao la kwanza
0 comments:
Post a Comment