KARIBU katika mechi ya gharama kubwa zaidi duniani – wachezaji 22 wa bei mbaya zaidi daima wenye thamani ya Pauni Milioni 417 kuumana uwanjani... Barcelona wanaikaribisha Real Madrid leo Jumamosi katika El Clasico ya kwanza msimu huu: Messi v Ronaldo, Neymar v Bale, Pique v Ramos.
Huku timu ya Carlo Ancelotti ikizidiwa pointi tatu na kikosi cha Gerardo Martino katika La Liga, kipigo kitatengeneza tofauti kubwa baina ya timu hizo mwanzoni mwa msimu.
Katika miaka ya karibuni imekuwa mechi ya mchuano mkali, ufundi, na mabao.
Wanawafukuzia: Real wapo nafasi ya tatu, wakiwa wameshinda mechi saba, sare moja na kufungwa moja katika mechi tisa
Barcelona (4-1-2-3)
Victor Valdes – Akademi
Alitarajiwa kuondoka Nou Camp msimu huu bada ya Monaco kutoa ofa kubwa ya kumnunua na Pepe Reina akatajwa kuja kuziba pengo lake, lakini kipa huyo mwenye umri wa miaka 31 amebaki na amedaka mechi saba bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa msimu huu katika mechi 12. 7/10.
Namba 1: Valdes (kushoto) ni kipa anayeheshimika Ulaya
Dani Alves - Pauni Milioni 23
Bila shaka ndiye beki bora zaidi wa kulia duniani. Anafahamika zaidi kwa shughuli yake uwanjani, akipanda kusaidia mashambulizi na kuzuia kwa ustadi mkubwa. 9
Mtaalamu: Kama Marcelo wa Real, Alves anapanda kushuka
Gerard Pique - Pauni Milioni 5
Katika kitabu chake binafsi, Sir Alex Ferguson amemtaja beki huyo wa kati mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4 kwamba bora katika kutoa pasi na anahamasisha ushindi. Anasifika na kuheshimika sana awapo uwanjani popote. 9
Beki mstaarabu: Pique alisajiliwa tena kutoka Manchester United kwa Pauni Milioni 5
Carles Puyol - Akademi
Akiwa na umri wa miaka 35 anaweza kuonekana mzee, lakini sentahafu huyo aliyeichezea mechi 100 Hispania bado ana mengiya kufanya, kwa ujumla katika mechi za wapinzani hao wa Hispania. Ni mzoefu na anajua kuongoza vyemka jahazi la timu yake. 8
Mr Barcelona: Ana umri wa miaka 35, lakini uzoefu wa Puyol ni muhimu katika El Clasicos
Adriano - Pauni Milioni 8.1
Adriano - Pauni Milioni 8.1
Akiwa amepunguziwa mshahara kwa pauni 77, Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 28 anafahamika kama ‘Utility Man’ na tovuti ya Barca. Beki wa kushoto chaguo la kwanza aliyefunga mabao mawili msimu huu. 7
Mpiganaji: Beki mwingine anayeshambulia sana, Adriano atakimbiza sana kwenye winga yake leo
Sergio Busquets – Akademi
Ana kila sababu ya kuitwa mchezaji mkubwa baada ya mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo huo. Kiungo huyo tegemeo wa Barcelona ana Medali za Dhahabu za Kombe la Dunia, Ubingwa wa Ulaya na Kombe la Ulaya. 9
Mtu wa kazi: Busquets ni kiungo muhimu Barca
Xavi – Akademi
Mtaalamu wa tiki-taka akiwa na Medali za kutosha bado ni mtu muhimu ndani ya Barca hususan katika mechi kama hizi. Akiwa na umri wa miaka 33 bado anaonekana yuko vizuri na hana dalili za kuchuja hata kesho. 9
Mtu wa kazi: Akili ya Xavi kimchezo inamaanisha yeye no bora sana
Andres Iniesta – Akademi
Pacha huyo wa Xavi katikati ya Uwanja akiwa anazidiwa miaka minne na mwebnzake huyo, anaweza kuchukua maukumu mara mkongwe huyo atakapoondoka. Ni mtaalamu wa kutengeneza mabao. 9
Kaka wa kambo: Mtu wa kulia wa Xavi, Iniesta ana muda zaidi wa kucheza Barca
Alexis Sanchez - Pauni Milioni 22
Winga huyo wa Chile alifahamika duniani baada ya Kombe la Dunia mwaka 2010. Bado hajafikia haswa ubora ule wa Barca, lakini anaweza kucheza katika timu hiyo. 8
Winga: Sanchez anahitaji mechi zaidi ili kulata uzoefu na kufikia ubora wa Barca
Neymar - Pauni Milioni 48.6
Hatimaye ametua Barca msimu huu kuunda safu ya ushambuliaji na mkali mwenzake kutoka Amerika Kusini, Messi. Akiwa amefunga mabao mawili tu hadi sasa, atapenda kuweka kumbukumbu zake katika mechi yake ya kwanza wapinzani hao kucheza. 9
Mchezaji ghali: Neymar amezoea haraka Nou Camp baada ya kununuliwa kwa Pauni Milioni na Barcelona kutoka Santos ya Brazil
Lionel Messi – Akademi
Nini zaidi unaweza kusema? Hizi ni baadhi ya takwim: Amefunga mabao 18 na kutoa pasi za mabao 11 katika mechi 25 zilizopita za El Clasicos. Huwa mtu mwingine kabisa anapocheza dhidi ya Madrid. 10
Hakuna cha kusema zaidi: Messi anapedna kucheza dhidi ya Madrid, na amefunga mabao 18 katika El Clasicos
JUMLA YA GHARAMA: Pauni Milioni 106.7.
VIWANGO KWA UJUMLA: 94/110
VIWANGO KWA UJUMLA: 94/110
Real Madrid (4-2-3-1)
Diego Lopez - Pauni Miloni 3
Alianza kupewa nafasi na Jose Mourinho badala ya Iker Casillas na Ancelotti amefuata utaratibu huo. Kipa huyo hodari mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 ni mahiri mno kuokoa michomo. 8/10
Kuelekea mechi: Lopez amempindua gwiji wa Real, Iker Casillas kuwa kipa wa kwanza klabu hiyo
Alvaro Arbeloa - Pauni Milioni 5
Ni chaguo la kwanza katika beki ya kulia tangu arejee mwaka 2009 katika klabu hiyo aliyojiunga nayo awali akiwa kinda. Beki huyo wa zamani wa Liverpool ni nguzo imara katika safu ya ulinzi ya Real. 7
Kisiki: Beki hodari wa kulia aliyeishika beki ya kulia kwa miaka michache iliyopita
Sergio Ramos - Pauni Milioni 23
Beki asiye na mambo mengi ambaye anatulia na mpira hakika bado ni mtu muhimu katika klabu hiyo. Katika msimu wake wa tisa Bernabeu ni mtu mwenye uzito ndani ya chumba cha kubadilishia nguo cha Real. 9
Mtu mzima: Ramos anaunganisha na kuleta umoja ndani ya kikosi, na ana misimu tisa katika klabu hiyo
Raphael Varane - Pauni Milioni 8.5
Beki wa kati mwenye ufundi wa hali ya juu, alijihakikishia namba kikosi cha kwanza baada ya kucheza vizuri kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa, Real ikiifunga Manchester City msimu uliopita. Akiwa ana umri wa miaka 20, anaweza kuja kuwa beki wa kati tegemeo wa Madrid miaka ijayo. 8
Kinda hatari: Akiwa na umri wa miaka 20, Varane (kulia) anaweza kuwa tegemeo la Bernabeu baadaye
Marcelo - Pauni Milioni 5.4
Mbrazil huyo anashambulia zaidi katika beki ya kushoto, ingawa pia anafanya vizuri kazi yake ya ulinzi na ana uzoefu sasa wa mechi za wapinzani. 8
Safi: Marcelo anashambulia zaidi
Asier Illarramendi - Pauni Milioni 34
Mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa dau la kiwango cha kati, akiwa ana umri wa miaka 23 ameonyesha ni kiungo hodari mkabaji aliyesajiliwa kutoka Real Sociedad msimu huu na ameingia kwenye kikosi cha kutokana na Xabi Alonso kuwa majeruhi, lakini amedhihirisha ubora wake. 8
Presha: lllarramendi aliigharimu Madrid Pauni Milioni 34 kutoka Real Sociedad msimu huu
Sami Khedira - Pauni Milioni 12
Huyu ni tegemeo la safu ya kiungo ya Madrid. Anaichezesha timu vizuri na kuvunja mashambulizi ya timu pinzani. Unaweza kumuita kiungo mmoja bora ambaye anaifanya Real iwe imara. 8
Mashine: Khedira anaiongoza vyema safu ya kiungo ya Real
Gareth Bale - Pauni Milioni 86
Akiwa amefunga mwanzoni, lakini mchezaji huyo ghali duniani amekuwa na mwanzo mgumu Real kutokana na kuandamwa na majeruhi yanayomuweka nje ya kikosi cha timu hiyo kwa muda mrefu. Yuko tayari kucheza El Clasico yake ya kwanza. 9
Anajipanga: Bale amekuwa na mwanzo mgumu Real, lakini anatarajiwa kucheza leo Nou Camp
Isco - Pauni Milioni 23
Isco - Pauni Milioni 23
Moja ya sababu za Mesut Ozil kuondoka katika klabu hiyo, Mchezaji huyo namba 10 wa Hispania alikataa ofa ya Manchester City ili kujiunga na timu hiyo msimu huu. Ameanza na moto akiwa amefunga mabao mabao matano katika mechi sita. 8
Hiki kifaa: Isco alitakiwa na klabu kadhaa tajiri na kubwa duniani msim huu, lakini akachagua
Cristiano Ronaldo - Pauni Milioni 80
Ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao katika mechi sita mfululizo za El Clasicos. Amefunga mabao 18 katika mechi 14 za klabu na timu yake ya taifa msimu huu. 10
Mkali kweli: Ronaldo inaelezwa yupo katika kiwango cha juu zaidi maishani mwake katika miaka mitatu iliyopita
Karim Benzema - Pauni Milioni 30
Mshambuliaji wa kati wa Real asiyepinka kwa sasa baada ya Gonzalo Higuain kuondoka, lakini akiwa amefunga mabao manne katika mechi 11 msimu huu anaweza kuanza ili adhihirishe makali yake na kuisaidia timu leo. 8
Mtu wa juu: Benzema (kushoto) sasa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Real baada ya kuondoka kwa Higuain msimu uliopita
JUMLA YA GHARAMA: Pauni Milioni 309.9m
VIWANGO KWA UJUMLA: 91/110
0 comments:
Post a Comment