IMEWEKWA OKTOBA 2, 2013 SAA 10:40 USIKU
MABAO mawili ya Ramires moja kila kipindi, moja la wenyeji kujifunga na moja la Frank Lampard yamempa furaha kocha Mreno, Jose Mourinho baada ya Chelsea kuichapa Steaua Bucharest mabao 4-0 katika Ligi ya Mabingwa usiku huu.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Terry, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Oscar/Azpilicueta, Mata/Willian dk80, Schurrle na Torres/Eto'o dk11.
Steaua: Tatarusanu, Georgievski/Varela dk71, Szukala, Gardos, Latovlevici, Bouceanu, Filip, Popa/Kapetanos mapumziko, Stanciu, Tanase na Piovaccari/Tatu mapumziko.
Mawili: Ramires akishangilia bao lake la pili katika ushindi wa 3-0 wa Chelsea
Ramires akifunga bao lake la pili
Fernando Torres alitolewa nje baada ya kuumia dakika ya 11 na nafasi yake kuchukuliwa na Samuel Eto'o
Ramires akifunga bao la kwanza kabla ya kwenda kushangilia na Juan Mata (chini)
Bado wamo: Shuti la Samuel Eto lilimbabatiza mchezaji wa Steaua akajifunga
Pati la ushindi: Frank Lampard (kushoto) akishangilia bao lake la dakika za majeruhi lililohitimisha ushindi mnono wa 4-0
Katika mchezo mwingine, bao pekee la Fabregas dakika ya 75 lilitosha kuipa ushindi wa ugenini, Barcelona wa 1-0 dhidi ya Celtic nchini Scotland.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra, Adriano, Xavi, Busquets, Iniesta, Fabregas/Tello dk78, Pedro/Sanchez dk74 na Neymar.
Celtic: Forster, Lustig/Forrest dk70, van Dijk, Ambrose, Izaguirre, Matthews, Brown, Mulgrew, Samaras, Commons/Pukki dk86, Stokes/Kayal dk70.
Kichwa, nyavuni: Cesc Fabregas (chini) aliunganisha krosi ya Alexis Sanchez kumtungua Fraser Forster
Sherehe: Barcelona wakimpongeza mfungaji wa bao lao pekee, Fabregas
Anatisha: Fabregas akipiga ngumi hewani baada ya kuipa ushindi Barca
Katika mchezo mwingine, bao la dakika mwishoni mno la mkwaju wa penalti wa Mario Balotelli limeinsuru AC Milan kulala baada ya kupata sare ya 1-1 na Ajax katika Kundi H.
Waholanzi walifikiri wameshinda baada ya bao la kichwa la Stefano Denswil dakika ya 90, lakini kulikuwa kuna zali la Balotelli aliyechezewa rafu na Mike van der Hoorn kwenye eneo la hatari na mwenyewe akaenda kufunga kwa tuta..
Mkombozi: Mario Balotelli akifunga kwa penalty dakika za lala salama kuinusuru AC Milan kulala kwa Ajax
Fungeni midomo yenu: Mario Balotelli akipongezwa na wenzake kwa kazi nzuri
Schalke inaongoza kundi E kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Basel, bao pekee la Julian Draxler dakika ya 54.
Washindi wa pili wa msimu uliopita, Borussia Dortmund walipata pointi zao za kwanza baada ya kuifunga Marseille ambayo haina pointi hadi sasa mabao 3-0.
Dortmund iliyofungwa na Napoli wiki mbili zilizopita, ilipata mabao yake kupitia kwa Robert Lewandowski dakika ya 19 na 79 kwa penalti na Marco Reus dakika saba baada ya kuanza kipindi cha pili.