// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CAMEROON YANUSA KOMBE LA DUNIA BRAZIL MWAKANI, KIPA WA LIVERPOOL AWABEBA 'VIBAYA' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CAMEROON YANUSA KOMBE LA DUNIA BRAZIL MWAKANI, KIPA WA LIVERPOOL AWABEBA 'VIBAYA' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, October 13, 2013

    CAMEROON YANUSA KOMBE LA DUNIA BRAZIL MWAKANI, KIPA WA LIVERPOOL AWABEBA 'VIBAYA'


    Kipa Charles Itandje amekuwa shujaa leo

    KIPA wa zamani wa Liverpool, Charles Itandje amefanya zi nzuri leo kuisaidia Cameroon kulazimisha sare ya 0-0 ugenini na Tunisia katika mechi ya kwanza ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia, hatua ya mwisho.

    Baada ya kupewa nafasi ya pili kufuatia Cape Verde kuondolewa, Watunisia walishamulia sana dakika za mwanzoni, lakini wakakwamishwa na mlinda mlango mwenye umri wa miaka 30 mzaliwa wa Ufaransa.
    Nahodha wa Cameroon, Samuel Eto'o, alirejea uwanjani leo baada ya kustaafu kwa muda mfupi na alikuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Tunisia katika mechi hiyo ya kusaka tiketi ya Brazil mwakani.
    Timu hizo zitarudiana mjini Yaounde Novemba 17 na mshindi atakwenda Brazil.
    Katika mchezo mwingine leo, mabao mawili ya Emmanuel Emenike yameipa Nigeria ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Ethiopia, iliyotangulia kupata bao baada ya kipa na Nahodha wa Super Eagle, Vincent Enyeama kuipangulia nyavuni krosi ya Behailu Assefa.
    Katika mechi za jana, Burkina Faso ilishinda 3-2 nyumbani dhidi ya Algeria, wakati Ivory Coast ilishinda 3-1 nyumbani dhidi ya Senegal. Ghana itamenyana na Misri Jumanne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAMEROON YANUSA KOMBE LA DUNIA BRAZIL MWAKANI, KIPA WA LIVERPOOL AWABEBA 'VIBAYA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top