// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BRANDTS NI KIBOKO YA SIMBA SC, LAKINI KING KIBADEN NI HABARI NYINGINE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BRANDTS NI KIBOKO YA SIMBA SC, LAKINI KING KIBADEN NI HABARI NYINGINE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 17, 2013

    BRANDTS NI KIBOKO YA SIMBA SC, LAKINI KING KIBADEN NI HABARI NYINGINE

    NYASI za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zinatarajiwa kuwaka moto Jumapili kwa mpambano wa watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga. Huo utakuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na leo BIN ZUBEIRY inaendelea kukuletea mfululizo wa makala za kuelekea pambano hilo linalobeba picha halisi ya soka ya Tanzania. Sasa tunamgeukia kocha Mholanzi wa Yanga SC, Ernie Brandts na mechi dhidi ya Simba SC. Endelea.
    Kiboko ya Mnyama? Brandts atapambana na kocha wa tatu tofauti ndani ya mechi tatu dhidi ya Simba SC Jumapili

    Beki wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, Jumapili ataiongoza Yanga SC kwa mara ya tatu dhidi ya watani wa jadi, Simba SC tangu arithi mikoba ya Mbelgiji Tom Saintfiet Oktoba mwaka jana.
    Katika mech mbili za awali, Brandts alipambana na makocha wawili tofauti, kwanza Mserbia Milovan Cirkovick aliyetoa naye sare ya 1-1 na baadaye Mfaransa, Patrick Liewig aliyemfunga mabao 2-0 katika mchezo wa kuhitimisha msimu uliopita, Yanga SC ikikabidhiwa Kombe kwa raha zote- ushindi dhidi ya watani na ubingwa.
    Mholanzi huyo aliyetua Yanga SC akitokea APR ya Rwanda aliyoifundisha tangu 2010, Jumapili atapambana na kocha mwingine pia, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na Simba SC.
    Brandts anajivunia rekodi ya kutofungwa na Yanga SC, lakini hawezi kusahau kipigo cha 1-0 kutoka Kagera Sugar msimu uliopita, ambayo ilikuwa inafundishwa na King Kibaden, aliyeibuka kocha bora wa Ligi Kuu mwishoni mwa msimu.
    Brandt alilipa kisasi kwa Kibaden kwa ushindi wa 1-0 pia katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Brandts na Kibaden kila mmoja kamfunga mwenzake mara moja, lakini Mholanzi wa Yanga hajafungwa na Simba SC. 
    Kiboko ya Brandts; King Kibaden aliifunga Yanga ya Brandts akiwa Kagera Sugar

    Mtaalamu huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap.
    Brandts aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na pia alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978. 
    Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za Kombe la Dunia.
    Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
    Alipostaafu soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa 2008–2009.
    Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako alifanya kazi hadi mwaka jana alipohamia Jangwani. Je, Jumapili Brandts ataendelea kuwa kiboko ya Simba SC, au Kibaden atamkumbusha machungu ya Kaitaba mwaka jana? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRANDTS NI KIBOKO YA SIMBA SC, LAKINI KING KIBADEN NI HABARI NYINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top