Na Mahmoud Zubeiry, Tanga
HARUNA Moshi Shaaban ‘Boban’ amecheza Simba SC kwa muda mrefu tangu mwaka 2004 alipojiunga nayo kutoka Moro United ya Morogoro hadi msimu uliopita alipotemwa.
Msimu huu amejiunga na Coastal Union ya Tanga na jana alikutana kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake hiyo ya zamani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Boban alionyesha heshima kubwa kwa timu yake ya zamani, akianzia kwenye kusalimiana vizuri kwa bashasha na wachezaji wa timu hiyo na pia akacheza kiungwana dhidi ya timu hiyo.
Ilitokea tu kwa bahati mbaya katika kuwania mpira wa juu, aligongana na kipa Abbel Dhaira ambaye akaumia na kushindwa kuendelea na mchezo kipindi cha kwanza.
Lakini kwa ujumla, Boban alicheza kiungwana dhidi ya timu yake ya zamani, tofauti na ilivyotarajiwa kwamba angecheza kibabe kumaliza hasira zake za kutemwa.
Lakini mabeki wa Simba SC, haswa Gilbert Kaze ‘hakumchukulia poa’ Boban na alikuwa akimdhibiti vikali kiasi cha kumuangusha chini zaidi ya mara tatu na kumfanya hadi atembelelee magoti wakati fulani kama kichanga kinachojifunza kutembea kwa kuanza kutambaa.
Kuna wakati Boban aligombea mpira na Kaze akadondokea mdomo na kulamba vumbi la Mkwakwani, lakini bado aliinuka na kuendelea kucheza kiungwana katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bila kufungana.

![]() |
Chama langu hilo; Haruna Moshi 'Boban' akiwaangalia wachezaji wa Simba SC |
Boban alionyesha heshima kubwa kwa timu yake ya zamani, akianzia kwenye kusalimiana vizuri kwa bashasha na wachezaji wa timu hiyo na pia akacheza kiungwana dhidi ya timu hiyo.
Ilitokea tu kwa bahati mbaya katika kuwania mpira wa juu, aligongana na kipa Abbel Dhaira ambaye akaumia na kushindwa kuendelea na mchezo kipindi cha kwanza.
Lakini kwa ujumla, Boban alicheza kiungwana dhidi ya timu yake ya zamani, tofauti na ilivyotarajiwa kwamba angecheza kibabe kumaliza hasira zake za kutemwa.
![]() |
We ndiyo Tambwe siyo; Boban akisalimiana na Amisi Tambwe |
![]() |
We beki kweli? Boban akisalimiana na Kaze Gilbert |
![]() |
Ukinifunga nitakununulia shampoo ya kuoshea rasta zako? Boban akisalimiana na Abbel Dhaira |
![]() |
Dogo unakomaa sasa; Boban akisalimiana na William Lucian 'Gallas' |
![]() |
We ndio kachaa wangu; Boban akisalimiana na Haruna Shamte |
Lakini mabeki wa Simba SC, haswa Gilbert Kaze ‘hakumchukulia poa’ Boban na alikuwa akimdhibiti vikali kiasi cha kumuangusha chini zaidi ya mara tatu na kumfanya hadi atembelelee magoti wakati fulani kama kichanga kinachojifunza kutembea kwa kuanza kutambaa.
Kuna wakati Boban aligombea mpira na Kaze akadondokea mdomo na kulamba vumbi la Mkwakwani, lakini bado aliinuka na kuendelea kucheza kiungwana katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bila kufungana.
![]() |
Ptu ptu ptu; Boban akitema vumbi baada ya kuangukia mdomo, huku akitambaa kuinuka kama kichanga kichanga, baada ya kuangushwa na Kaze Gilbert |
![]() |
Mpira uko wapi? Boban baada ya kuangushwa na Kaze |
![]() |
Sasa umejua mimi ni beki kweli; Boban akiangukia mpira baada ya kukumbana na Kaze Gilbert |
0 comments:
Post a Comment