// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BLATTER AMUOMBA RADHI RONALDO BAADA YA KUMKANDIA NA KUSEMA ANAMPENDA MESSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLATTER AMUOMBA RADHI RONALDO BAADA YA KUMKANDIA NA KUSEMA ANAMPENDA MESSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 29, 2013

    BLATTER AMUOMBA RADHI RONALDO BAADA YA KUMKANDIA NA KUSEMA ANAMPENDA MESSI

    RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter ameomba radhi kwa Cristiano Ronaldo baada ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid kumchamba katika ukurasa wake wa  Facebook.
    Mapema Blatter alitoa hotuba iliyomkera Ronaldo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza. Katika majadiliano yake na wanafunzi hao, Blatter alielezea mapenzi yake kwa Lionel Messi, na akaweka kando kiti chake cha Urais FIFA na kumshambulia kibinafsi Ronaldo. Blatter pia amesemekana kumpiga dongo nyota huyo wa Madrid kwamba anatumia fedha zake nyingi kupamba nywele zake.
    Hiyo imemfanya Mreno huyo, aliyeingizwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2013, Ballon d'Or, aposti katika ukurasa wake wa Facebook: "Video hii inaonyesha dhahiri heshima na namna ambavyo FIFA wapo kwangu, kwa klabu yangu na nchi yangu,". 
    VIDEO Kaangalie Sepp Blatter akimshambulia binafsi Cristiano Ronaldo

    Amefunguka: Ronaldo amejibu kauli za Blatter alizotoa wakati akizungumza na wanafunzi wa Oxford 
    Mocking: Blatter gets out of his chair during a discussion at Oxford Union and impersonates Ronaldo
    Ameboa: Blatter aliachia kiti chake alipokuwa Oxford na kumshambulia kibinafsi Ronaldo
    cr7 facebook.JPG
    Sepp Blatter

    Sepp Blatter

    ALIYOYASEMA SEPP BLATTER JUU YA MESSI v RONALDO KWA WANAFUNZI WA OXFORD

    "Wote ni wachezaji wa kipekee, lakini wako tofauti kabisa. Ni nyota tofauti kabisa. 
    "Lionel Messi ni kijana mzuri, ambaye kila baba na kila mama angependa kumpeleka nyumbani. Ni mtu mzuri, ana kasi sana, na anacheza vizuri. Ni mtu wa aina hiyo, kijana mzuri. Kitu ambacho kinamfanya awe maarufu, na kiasili wakati wote ataendelea kupata kura nyingi kwa sababu anacheza vizuri na kufunga mabao. 
    "Mwingine mmoja naye (Ronaldo) ni kitu fulani pia. Ni kama kamanda anavyocheza uwanjani. (Blatter akawa anaonyesha mifano ya uchezaji wake na kushangiliwa).
    "Huu ni upande mwingine wa soka na vizuri kuwa na makamanda uwanjani. Hawashibihiani na hicho ndicho kinaubeba mchezo wa soka. Mmoja anatumia fedha nyingi kutengeneza  nwele zaidi ya mwingine, lakini hiyo haijalishi. 
    "Siwezi kusema nani ni bora- kutakuwa na shindano mwaka huu tena Ballon d'Or. Nawapenda wote, lakini nampenda Messi,".


    "Mambo hadharani sasa. Namtakia Bwana. Blatter afya na maisha marefu, aendelee kuona na kushuhudia mafanikio ya timu na wachezaji anaowapenda,".
    Baadaye Blatter akaandika kwenye Twitter: "Dear @Cristiano. Naomba radhi kwako kama ulichukizwa na jibu la swali wangu katika tukio binafsi Ijumaa. Sikuwa na maana ya kukuumiza wewe.
    "Nina heshima Real Madrid @cristiano na tuna vipaji vingi katika mchezo huu duniani, ukiwemo wewe. Kila heri,". 
    Hatua hii inakuja baada ya Real Madrid kuiandikia FIFA ikimtaka Blatter aome radhi kwa maneno yake juu ya Ronaldo.
    Katika mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Sevilla, kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti amesema: "Rais [Florentino Perez] ametuma barua FIFA kumtaka Blatter kuomba radhi kwake kauli zake juu ya Cristiano.'
    Sorry Sepp: Blatter's two-part apology to Ronaldo
    Sorry Sepp: Blatter's two-part apology to Ronaldo
    Blatter tweet

    Training: Ronaldo (left) alongside Gareth Bale as Real Madrid prepare for Wednesday's match against Sevilla
    Mazoezi: Ronaldo (kushoto) akiwa mchezaji mwenzake Gareth Bale wakati Real Madrid ikijiandaa na mechi ya kesho na SevillaRivals: Blatter says he prefers Barcelona forward Messi (front) to Ronaldo
    Wapinzani: Blatter amesema anampenda mshambuliaji wa Barcelona, Messi (mbele) kuliko Ronaldootti: Maelezo ya Blatter kwa Ronaldo hayana heshima
    Demand: Real Madrid president Florentino Perez (right) has written a latter to FIFA asking for an apology
    Hasira: Rais wa Real Madrid, Florentino Perez (kulia) ameiandikia FIFA kuitaka iombe radhi
    Speech: Blatter appeared in front of students at the Oxford Union on Friday night
    Hotuba: Blatter alikuwa mbele ya wanafunzi wa Oxford Ijumaa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BLATTER AMUOMBA RADHI RONALDO BAADA YA KUMKANDIA NA KUSEMA ANAMPENDA MESSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top