Na Nurat Mahmoud, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa kampuni ya Bin Slum, wafadhili wa Coastal Union ya Tanga, Nassor Bin Slum leo amefiwa na baba yake mzazi jana, aliyekuwa amelazwa kwa matibabu katika hospitali ya Apollo mjini Hyderabad nchini India.
“Alhamdulillah mzee wangu KIPENZI tumempumzisha katika maisha yake mapya kabisa ya kaburini, saa kadhaa zilizopita jijini Hyderabad India, shukrani kwa ndugu zangu wa Tanzania na Kenya wanaosoma huku, kwani walinifanya nione msiba kama umetokea nyumbani tu.
“Lakini pia ndugu, jamaa na marafiki wote walionyesha kuguswa na msiba huu, kwani maombi yenu kwa mzee wangu na wetu sijui hata nimjibu au kumshukuru nani kwa kuguswa na msiba huu, kutoka moyoni mwangu, nasema asanteni sana sana kwa kunifanya nijione kumbe nyinyi ni familia yangu tusiyojuana baadhi yetu.
“Sioni cha kuwalipa, kwa jinsi mlivyonifariji, ila niwaambie, Mungu ndiye mlipaji bora kabisa katika walipaji,”alisema Nassor katika taarifa yake kwenye ukurasa wa wa facebook.
Mapema juzi, Nassor alizungumza na BIN ZUBEIRY kutoka hospitali ya Apoloo, Hyderabad City kuhusu afyaya mzee wake na juu ya kufanyiwa kwake upasaji mdogo wa goti.
Bin Slum ambaye hucheza soka katika timu yake ya maveterani inayofanya mazoezi Uwanja wa shule ya Msingi Muhimbili, Dar es Salaam, alisema anaendelea vizuri baada ya upasuaji huo.
Nassor alisema kwamba aliwahi kufanyiwa upasuaji kama huo katika hospitali ya TMJ mjini Dar es Salaam miaka 15 iliyopita na hajawahi kupata maumivu makubwa tena tangu wakati huo, pamoja na kucheza soka ya ushindani kipindi chote hicho hadi miaka mitano iliyopita alipostaafu na sasa anacheza kwa kujifurahisha.
Kuhusu baba yake, alisema; “Mzee wangu kwa mwezi mzima nipo naye huku, kwa kweli hali yake si nzuri, na yupo chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), kwa kweli nakabiliwa na mtihani sana, nipo katika wakati mgumu sana,”alisema, ambaye baba yake ana umri wa miaka 78. Mungu aiweke pema peponi roho yake amin.

Pole swahiba; Bin Slum amefiwa na baba yake mzazi India |