// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BERGKAMP ATAKA KUREJEA ARSENAL KUPIGA KAZI, PIRES TAYARI ANAMPIGA 'TAFU' WENGER - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BERGKAMP ATAKA KUREJEA ARSENAL KUPIGA KAZI, PIRES TAYARI ANAMPIGA 'TAFU' WENGER - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 09, 2013

    BERGKAMP ATAKA KUREJEA ARSENAL KUPIGA KAZI, PIRES TAYARI ANAMPIGA 'TAFU' WENGER

    GWIJI wa Arsenal, Dennis Bergkamp ameelezea nia yake ya kujiunga na dawati la makocha la timu ya Arsene Wenger.
    Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 44 alunga mabao 87 katika miaka yake 11 ya kuchezea Arsenal na amesema klabu hiyo ina nafasi maalum moyoni mwake.
    Robert Pires amekuwa akisaidia kuendesha mazoezi katika Uwanja wa Gunners, London Colney na Bergkamp, ambaye aliichezea timu hiyo kuanzia mwaka 1995 hadi2006, anaweza kuungana naye.
    Deadly Dutchman: Dennis Bergkamp celebrates scoring for Arsenal against Blackburn Rovers in 2002
    Mholanzi hatari: Dennis Bergkamp akishangilia kuifungia Arsenal dhidi ya Blackburn Rovers mwaka 2002Welcome return: Former Arsenal star Robert Pires recently returned to the Gunners to assist with training session
    Karibu tena: Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Robert Pires hivi karibuni amerejea The Gunners kusaidia kuongoza mazoezi
    "Hisia alizonazo Johan Cruyff kwa Barcelona, nami ninazo hizo hizo kwa Arsenal," Bergkamp aliiambia Telegraph.
    "Nikiwa Arsenal ilikuwa babu kubwa. Wakati wote nafurahia. Sijawahi kuwa na siku mbaya humo. Ipo katika fikra zangu wakati wote. Ni sehemu ya malengo yangu kurejea huko. 
    "Naona kama naweza kuwa sehemu ya makocha. Nafurahia hiyo kazi, hususan kufundisha vitu binafasi kwa washambuliaji,".
    Bergkamp alijipatia sifa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka, ubunifu na maarifa ya kisoka alipokuwa Arsenal.
    Dream team: Sol Campbell, Freddie Ljungberg, Thierry Henry, Dennis Bergkamp and Robert Pires during a training session in 2004
    Timu la kukumbukwa: Sol Campbell, Freddie Ljungberg, Thierry Henry, Dennis Bergkamp na Robert Pires wakiwa mazoezini mwaka 2004
    Invincibles: Dennis Bergkamp shows of the Premier League trophy during a victory parade through Islington in 2004
    Mkali kweli: Dennis Bergkamp akiwa na taji la Ligi Kuu ya England mwaka 2004
    Mchezaji mpya ghali wa Arsenal, Mesut Ozil amekuwa akifananishwa na Mholanzi huyo, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi amesema kila mchezaji ni wa kipekee.
    Sasa akiwa kocha Msaidizi wa Ajax, Bergkamp amevutiwa na mwanzo mzuri wa Arsenal msimu huu na kusema Ozil ni kipaji maalum.
    "Pamoja na heshima zangu zote kwa wachezaji wengine wote wa Arsenal, nafikiri ni mmoja ambaye anaweza kutengeneza tofauti,"alisema. 
    "Wachezaji wengine ni wazuri katika kiungo. Lakini unahitaji mtu mmoja fulani wa kiwango cha juu ambaye anaweza kuhaha Uwanja mzima,". 
    Summer signing: Arsenal's new recruit Mesut Ozil has drawn comparisons with Dennis Bergkamp
    Mchezaji mpya: Mchezaji mpya ghali wa Arsenal, Mesut Ozil anwakumbusha mashabiki wa timu hiyo enzi za Dennis Bergkamp
    Hot shots: Arsenal team-mates Thierry Henry and Dennis Bergkamp celebrate a goal against Everton in 2004
    Wakali watupu: Wachezaji wa Arsenal, Thierry Henry na Dennis Bergkamp wakishangilia bao dhidi ya Everton mwaka 2004
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BERGKAMP ATAKA KUREJEA ARSENAL KUPIGA KAZI, PIRES TAYARI ANAMPIGA 'TAFU' WENGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top