IMEWEKWA OKTOBA 1, 2013 SAA 4:32 USIKU
MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich wametua katika ardhi ya England tayari kwa mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City kesho.
'Walume' wa Pep Guardiola walianza vyema kampeni ya kutetea taji lao baada ya kuichapa mabao 3-0 CSK Moscow na kesho wanatarajiwa kuendeleza wimbi la ushindi.
Kuwasili kwao katika Uwanja wa Ndege wa Manchester leo kuliteka hisia za wengi kuliko walivyotua England mara ya mwisho mjini London kwa ajili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita dhidi ya wapinzani wao wa Bundesliga, Borussia Dortmund mechi waliyoshinda Uwanja wa Wembley na kutwaa taji.
Lakini baada ya City pia kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Viktoria Plzen mabao 3-0, kocha wa zamani wa Barcelona wazi atakuwana na wapinzani kweli katika kundi lake, D kesho.
Tishio: Winga wa kimataifa wa Uholanzi, Arjen Robben akiwasili Uwanja wa Ndege wa Manchester kwa ajili ya mechi ya timu yake, Bayern ya Ligi ya Mabingwa kesho
Shabiki wa kweli: Nyota wa Bayern, Bastian Sweinsteiger alipata mapokezi mazuri kuelekea mechi ya kesho Uwanja wa Etihad
Mfululizo: Bayern Munich wamepania kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa
Burudani katika mchezo huo inachangiwa na kauli ya kocha wa Man City, Manuel Pellegrini aliyesema ataingiza kikosi chake kugombea pointi tatu, licha ya ukweli wa vipaji viliyosheheni Bayern.
"Bayern ni wagumu sana, lakini pia tuko katika wakati mzuri, hivyo tunaweza kuvuna pointi tatu,"alisema kocha huyo mwenye uzoefu wa kutosha wa Ligi ya Mabingwa kuanzia timu za Villareal, Real Madrid na Malaga nchini Hispania
Mvuto wa nyota: Mfaransa Frank Ribery na Mjerumani Mario Gotze waling'ara katika mapokezi na kusaini autograph kibao
Ngongoti: Beki wa Bayern, Daniel van Buyten aliichezea mechi tano Man City alipokuwa kwa mkopo kutoka Marseille mwaka 2004
Mabingwa wa Ulaya: Bayern walisafirisha basi la timu yao kutoka Munich hadi Manchester Jumapili
Anahitaji mtaji: Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola alikuwa kivutio pia kama wachezaji wake wakati timu hiyo ilipowasili Manchester
Changamoto: Guardiola alirithi mikoba ya Jupp Heynckes aliyeipa Bayern taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita Uwanja wa Wembley