• HABARI MPYA

        Tuesday, October 29, 2013

        BALE AINGIA KINYANG'ANYIRO TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA NA MESSI, RONALDO...VAN PERSIE YUMO PIA

        WINGA  wa Wales, Gareth Bale ameungana na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo katika washindani wa juu wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, maarufu kama Ballon d'Or.
        Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameingia kwenye orodha ya wanasoka wanaowania ufalme wa dunia, iliyotolewa leo ambayo mshindi wake atatajwa Januari 13 mwakani mjini Zurich, Uswisi

        Hot shot: Robin Van Persie fired Manchester United to the Premier League title last season
        Record breaker: Gareth Bale made a £86m move to Real Madrid following a superb season for Tottenham

        Record breaker: Gareth Bale made a £86m move to Real Madrid following a superb season for Tottenham

        Hit man: Luis Suarez has been sensational for Liverpool
        Hit man: Luis Suarez has been sensational for Liverpool

        ORODHA YA WANAPOWANIA BALLO D'OR

        Gareth Bale (Real Madrid/Wales)
        Philipp Lahm (Bayern Munich/Germany)
        Thomas Muller (B Munich/Germany) 
        Manuel Neuer (B Munich/Germany) 
        Bastian Schweinsteiger (B Munich/Germany)
        Mesut Ozil (Arsenal/Germany)
        Robin van Persie (Man United/Netherlands)
        Arjen Robben (B Munich/Netherlands) 
        Edinson Cavani (PSG/Uruguay)
        Luis Suarez (Liverpool/Uruguay)
        Andres Iniesta (Barcelona/Spain)
        Xavi (Barcelona/Spain)
        Neymar (Barcelona/Brazil)
        Thiago Silva (PSG/Brazil)
        Radamel Falcao (Monaco/Colombia)
        Andrea Pirlo (Juventus/Italy)
        Franck Ribery (B Munich/France)
        Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal)
        Eden Hazard (Chelsea/Belgium)
        Zlatan Ibrahimovic (PSG/Sweden)
        Robert Lewandowski (Dortmund/Poland)
        Lionel Messi (Barcelona/Argentina)
        Yaya Toure (Manchester City/Ivory Coast)

        Bale, alijiunga na Real Madrid akitokea Tottenham kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 86, Septemba baada ya kuifungoa mabao 26 Spurs msimu uliopita.
        Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina, Messi amekuwa akishikilia tuzo hiyo kwa miaka minne iliyopita, na mchezaji mwenzake Bale ndani ya Madrid, Ronaldo amekuwa wa pili miaka yote hiyo.
        Franck Ribery, ambaye ameshinda tuzo ya Mwanasoka bora wa Ulaya ya UEFA msimu  wa 2012-13, baada ya kuisaidia Bayern Munich kushinda mataji la Ligi ya Mabingwa, Bundesliga na Kombe la Ujerumani, ni mchezaji mwingine mwenye jina kubwa katika orodha hiyo.
        Ribery anaungana na wachezaji wenzake wa Bayern, Philipp Lahm, Thomas Muller, Manuel Neuer, Arjen Robben na Bastian Schweinsteiger wakati pia nyota wa Barcelona, Xavi, Andres Iniesta na Neymar aliyesajiliwa msimu huu wamo.
        Wachezaji watatu wa Paris St Germain, Zlatan Ibrahimovic, Edinson Cavani na Thiago Silva wamo pia pamoja  na nyota mwingine mwenye jina kubwa Ligue 1 ya Ufaransa, Radamel Falcao wa Monaco aliyesajiliwa kuoka Atletico Madrid msimu huu.
        Pamoja na orodha hiyo ndefu, bado katika tuzo hizo wanasoka wawili wapinzani wakubwa, Ronaldo na Messi wanatarajiwa kutawala kutokana na kuonekana kwamba bado wako juuu ya wengine
        Talisman: Manchester City midfielder Yaya Toure
        Talisman: Manchester City midfielder Yaya Toure
        Tricky: Chelsea's Eden Hazard
        Tricky: Chelsea's Eden Hazard
        Wizard: Mesut Ozil has continued his fine form at Arsenal following summer switch from Real Madrid
        Wizard: Mesut Ozil has continued his fine form at Arsenal following summer switch from Real Madrid
        Main challenger: Real Madrid's Cristiano Ronaldo
        Main challenger: Real Madrid's Cristiano RonaldoSimply the best: Lionel Messi has won the award for the past four years
        Simply the best: Lionel Messi has won the award for the past four years
        Barcelona's forward Lionel Messi
        Sir Alex Ferguson
        Rafael Benitez
        Rivals: Sir Alex Ferguson (left) and Rafael Benitez (right) are up for coach award
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: BALE AINGIA KINYANG'ANYIRO TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA NA MESSI, RONALDO...VAN PERSIE YUMO PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry