// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM HAIISHI MAJERUHI, HIMID MAO NAYE AKOROFISHA GOTI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM HAIISHI MAJERUHI, HIMID MAO NAYE AKOROFISHA GOTI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 01, 2013

    AZAM HAIISHI MAJERUHI, HIMID MAO NAYE AKOROFISHA GOTI

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA OKTOBA 1, 2013 SAA 5:25 ASUBUHI
    AZAM haiishi bila majeruhi! Siku chache baada ya kupona kwa majeruhi wa muda mrefu wa Azam FC, Brian Umony, John Bocco na Humphrey Mieno, mchezaji mwingine tegemeo wa timu hiyo kwa sasa, Himid Mao naye ameumia.
    Kiungo Mkenya, Mieno na washambuliaji Mganda, Umony na mzalendo Bocco maarufu kama Adebayor walikuwa majeruhi kwa muda mrefu, lakini wiki iliyopita wakapona na kuanza kucheza.
    Sasa kocha Muingereza, Stewart Hall amepoteza silaha yake nyingine muhimu, Himid ambaye amekuwa akiongoza safu ya kiungo tangu mwanzo wa msimu.
    Pigo Azam; Himid Mao ameumia goti

    Mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Pamba SC ya Mwanza, Mao Mkami ‘Ball Dancer’ aliumia goti la mguu wa kulia siku mbili kabla ya mechi na Prisons mjini Mbeya.
    Meneja wa Azam FC, Jemadari Said ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Himid baada ya kuumia anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua uzito wa maumivu yake.
    “Daktari wa timu (Mwanandi Mwankemwa) alirejea Dar es Salaam tulivyotoka Mbeya, anatarajiwa kuungana na timu tena Tanga siku ya Alhamisi na amesema akifika hapa ndipo atampeleka Himid katika hospitali ya Bombo kufanyiwa uchunguzi,”alisema Jemadari.  
    Goti la Himid lililoumia

    Azam iliwasili Tanga jana majira ya saa moja usiku na kufikia katika hoteli ya Soni Inn, wakati leo inatarajiwa kufanya mazoezi katika Uwanja wa Popatlal, kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Coastal Union ya Tanga Jumamosi.
    Timu hizo ziliongozana zote Mbeya kwa mechi za mwishoni mwa wiki, Coastal ikitoa sare ya 1-1 na Mbeya City na Azam ikitoa sare ya 1-1 pia na Prisons, Uwanja wa Sokoine Jumapili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM HAIISHI MAJERUHI, HIMID MAO NAYE AKOROFISHA GOTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top