Na Princess Asia, Chamazi, Dar es Salaam
AZAM FC imeiengua Yanga SC katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 jioni hii dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa itimize pointi 17, baada ya kucheza mechi tisa, moja nyuma ya vinara Simba SC na mbili zaidi mbele ya mabingwa watetezi, Yanga.
Hata hivyo, Simba na Yanga zimecheza mechi nane nane kila moja tofauti na Azam ambayo imecheza mechi ya tisa ya leo.
Katika mchezo huo, mkali na wa kusisimua, mabao ya washindi wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita yaliwekwa kimiani na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 12, beki Erasto Nyoni dakika ya 39 na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 90.
Kwa ujumla, Azam inayofundishwa na Muingereza Stewart Hall, akisaidiwa na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Kali Ongala, ilicheza vizuri na kutawala sehemu kubwa ya mchezo wa leo.
Katika mechi nyingine za leo, Ruvu Shooting iliilaza bao 1-0 Rhino Rangers ya Tabora kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi, mkoani Pwani bao pekee la Elias Maguri dakika ya 77, hilo likiwa bao lake la tano msimu huu, akizidiwa matatu na Amisi Tambwe wa Simba SC anayeongoza kwa mabao yake saba.
Mbeya City iliyopanda Ligi Kuu msimu huu imeendeleza makali yake katika ligi hiyo kwa kuibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya wenyeji Mgambo Shooting, bao pekee la Jeremiah John dakika ya 20.
Mtibwa Sugar imefanya kufuru baada ya kuikung’uta mabao 5-2 JKT Oljoro Uwanja wa Manunu, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Mtibwa yalifungwa na Juma Luizio dakika ya tano na 31 na Abdallah Juma matatu dakika ya 23, 66 na 78.
Juma aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea Simba SC msimu huu amefunga hat trick ya pili msimu huu baada ya Tambwe wa Simba SC, wakati mabao ya Oljoro yamefungwa na Shaibu Nayopa dakika ya 72 kwa penalti na Amir Omar dakika ya 84.

Wauaji; Wafungaji wa mabao mawili ya Azam leo katika ushindi wa 3-0, John Bocco na Erasto Nyoni wakipongezana. Kushoto ni Aggrey Morris |
Hata hivyo, Simba na Yanga zimecheza mechi nane nane kila moja tofauti na Azam ambayo imecheza mechi ya tisa ya leo.
Katika mchezo huo, mkali na wa kusisimua, mabao ya washindi wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita yaliwekwa kimiani na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 12, beki Erasto Nyoni dakika ya 39 na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 90.
Kwa ujumla, Azam inayofundishwa na Muingereza Stewart Hall, akisaidiwa na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Kali Ongala, ilicheza vizuri na kutawala sehemu kubwa ya mchezo wa leo.
Katika mechi nyingine za leo, Ruvu Shooting iliilaza bao 1-0 Rhino Rangers ya Tabora kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi, mkoani Pwani bao pekee la Elias Maguri dakika ya 77, hilo likiwa bao lake la tano msimu huu, akizidiwa matatu na Amisi Tambwe wa Simba SC anayeongoza kwa mabao yake saba.
Kipre Tchetche akimtoka beki wa JKT Ruvu, Jamal Macheranga |
John Bocco akipambana na wachezaji wa JKT Ruvu kugombea mpira |
John Bocco akitafuta mbinu za kumtoka beki wa JKT Ruvu, Damas Makwaiya |
Mbeya City iliyopanda Ligi Kuu msimu huu imeendeleza makali yake katika ligi hiyo kwa kuibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya wenyeji Mgambo Shooting, bao pekee la Jeremiah John dakika ya 20.
Mtibwa Sugar imefanya kufuru baada ya kuikung’uta mabao 5-2 JKT Oljoro Uwanja wa Manunu, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Mtibwa yalifungwa na Juma Luizio dakika ya tano na 31 na Abdallah Juma matatu dakika ya 23, 66 na 78.
Juma aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea Simba SC msimu huu amefunga hat trick ya pili msimu huu baada ya Tambwe wa Simba SC, wakati mabao ya Oljoro yamefungwa na Shaibu Nayopa dakika ya 72 kwa penalti na Amir Omar dakika ya 84.
0 comments:
Post a Comment