// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ASHANTI UNITED WAANZA KULA RAHA LIGI KUU, WAICHAPA PRISONS 2-1 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ASHANTI UNITED WAANZA KULA RAHA LIGI KUU, WAICHAPA PRISONS 2-1 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 16, 2013

    ASHANTI UNITED WAANZA KULA RAHA LIGI KUU, WAICHAPA PRISONS 2-1 CHAMAZI

    Wachezaji wa Ashanti wakishangilia bao lao la ushindi leo Chamazi
    Na Mahmoud Zubeiry, Chamazi
    BAO la dakika ya 90 na ushei la Mwinyi Ally limeipa ushindi wa 2-1 Ashanti United dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mchezaji huyo aliyetokea benchi dakika ya 83 kuchukua nafasi ya Fakhi Hakika, alifunga bao baada ya kutokea kizazaa langoni mwa Prisons.
    Hadi mapumziko, tayari timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Prisons wakitangulia kupata bao dakika ya nne kupitia kwa John Matei na beki Tumba Sued akaisawazishia Ashanti dakika ya 21.
    Ibrahim Isaka wa Prisons kulia akipambana na Iddi Silas wa Ashanti United leo Chamazi

    Prisons inayofundishwa na kiungo wa zamani wa Simba SC, Jumanne Challe ilianza vyema mchezo huo dakika 10 za mwanzo, lakini baada ya hapo, upepo ukabadilika na Ashanti wakauteka mchezo.
    Ashanti wangeweza kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa wanaongoza kama si kukosa mabao ya wazi.
    Kipindi cha pili, Ashanti inayofundishwa na kiungo wa zamani wa Simba SC, Nico Kiondo iliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Prisons na kukosa mabao zaidi ya matatu ya wazi.
    Hussein Swedi aliyetokea benchi dakika ya 51 kuchukua nafasi ya Lusako Mwakyusa alikuwa mwiba mkali mbele ya mabeki wa Prisons, lakini alipoteza nafasi mbili za wazi na Paul Maona alipoteza nafasi moja.
    Kwa ushindi huo, Ashanti inatimiza point inane baada ya kucheza mechi tisa na sasa inasogea hadi nafasi ya 10 kutoka ya 13.
    Ashanti United; Daudi Mwasongwe, Hussein Mkongo/Anthony Matangalu dk46, Jaffar Gonga, Tumba Sued, Samir Ruhava, Iddi Silas, Mussa Nampaka, Fakhi Hakika/Mwinyi Allydk83, Paul Maona, Joseph Mahundi na Lusajo Mwakyusa/Hussein Swedi dk51.
    Prisons; Beno David, Salum Mashaka, Laurian Mpalile, Lugano Mwangama, Nurdin Issa/Frank William dk82, Omega Seme, John Matei, Freddy Chudu, Peter Michael, Hassan Isaka/Jumanne Elfadhil dk71 na Julius Kwanga/Jeremiah Juma dk47. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ASHANTI UNITED WAANZA KULA RAHA LIGI KUU, WAICHAPA PRISONS 2-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top