Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Oktoba 16 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ashanti United na Tanzania Prisons itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Nayo Ligi Daraja la Kwanza (FDL) nayo inaendelea kesho (Oktoba 16 mwaka huu) kwa mechi moja ya kundi A ambapo Polisi Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tessema kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekabidhi kitanda cha upasuaji kwa Hospitali ya Rufani ya Manispaa ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa jamii.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo (Oktoba 15 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF ambapo Hospitali ya Temeke iliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya hospitali hiyo James Syaga, Mganga Mkuu Dk. Amaani Malima na Matroni wa hospitali hiyo Deodata Msoma.
Akikabidhi kitanda hicho chenye thamani ya sh. milioni 6.8, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema amefurahi kuwa ahadi ya kukabidhi msaada huo wa Hospitali ya Temeke umetimia licha ya kuchukua muda mrefu kutokana na ukweli kuwa fedha za kununulia kitanda hicho zinatokana na mchezo wa Ngao ya Jamii wa mwaka jana kati ya Simba na Azam FC.
Alisema uamuzi wa kuiteua Hospitali ya Temeke ulitokana na ukweli kuwa pamoja na kwamba ofisi za TFF ziko wilayani Ilala, shughuli nyingi kubwa za Shirikisho linafanyika kwenye Manispaa ya Temeke na hivyo hospitali hiyo hufanya kazi kubwa ya kuhudumia watu mbalimbali wanaopata matatizo wakati wa michezo ya mpira wa miguu.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali, Dk. Malima aliishukuru TFF kwa kutimiza ahadi yao na kwamba msaada huo umekuja wakati muafaka kwa kuwa wana vyumba vitatu vya upasuaji, lakini ni viwili tu vilivyo na vitanda kwa hiyo kitanda hicho kitakamilisha chumba hicho kianze kufanya kazi.
Alisema Hospitali yake sio tu inahudumia wagonjwa kutoka wilayani Temeke, bali kutoka hata Mkoa wa Mtwara na sehemu nyingine zinazozunguka wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali, James Syaga, ambaye alisema anawakilisha watu wanaohudumiwa na Hospitali ya Temeke, alishukuru kwa msaada huo na kuiomba TFF kuendelea kuangalia uwezekano wa kusaidia hospitali hiyo.

Kikosi cha Prisons |

0 comments:
Post a Comment