KLABU ya Arsenal imejadili uwezekano wa kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Juventus, Fernando Llorente katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani.
Licha ya timu yake kuanza vizuri mwanzoni mwa msimu, kocha Arsene Wenger bado anataka kusajili mshambuliaji mpya.
Na The Gunners wapo karibu mno kufuatilia maendeleo ya mshambuliaji huyo wa Hispania mjini Turin kuelekea kumsajili mwanzoni mwa mwaka ujao.
Mambo hayaendi vizuri: Llorente alijiunga na Juventus mwanzoni mwa msimu, lakini amekosa namba ya uhakika kikosi cha kwanza
Wasaka vipaji wa Arsenal, walimuangalia Llorente kwa mapana marefu misimu ya karibuni na Wenger ni shabiki mkubwa wa mshambuliaji huyo.
Llorente alijiunga na Juventus akitokea Athletic Bilbao mwanzoni mwa msimu, lakini amekuwa akisotea namba kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa Carlos Tevez.
Na Arsenal inataka kutumia nafasi hiyo kwa kumuomba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa mkopo.
Llorente amepoteza nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania na inafahamika lazima apate namba ya kudumu katika klabu ili kujihakikishia nafasi ya kwenda na kikosi cha Vicente Del Bosque kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Anakimbizana na muda: Llorente amepoteza nafasi kikosi cha Hispania
Na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza Uwanja wa Emirates itakuwa nafasi ya kukata rufaa kwa Llorente kurejea kikosini Hispania.
Wakati huo huo, Wenger amesema kwamba yuko tayari kusaini Mkataba mpya na Arsenal.
BIN ZUBEIRY iliandika hivi karibuni kwamba klabu hiyo inataka kuanza mazungumzo ya Mkataba mpya na kocha huyo, ambao atakuwa analipwa Pauni Milioni 8 kwa msimu.
Mkataba wa sasa wa Wenger unaisha mwishoni mwa msimu na bilionea anayemiliki hisa nyingi za klabu hiyo, Stan Kroenke ameonyesha imani kubwa kwa kocha huyo na atanataka abaki.
Na Mfaransa huyo amesema anataka kustaafu masuala ya soka akiwa na klabu hiyo ya England.
Atabaki: Wenger ameelezea nia yake ya kubaki Arsenal
"Naweza kuyashuhudia maisha yangu yaliyobaki nikiwa England, kwa nini hapana?," alisema.
"Najisikia vizuri katika nchi hii, kwa sababu tunachangia hisia zetu za soka na napenda kuwashukuru sana nchi hii kwa kunikubali na kunipa nafasi. Nina furaha katika Uwanja wa mpira,".
Kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Santi Cazorla ameanza mazoezi yake baada ya kupona maumivu ya kifundo cha mguu.
Mspanyola huyo amekosekana kwa kiasi cha mwezi kutokana na maumivu hayo, lakini sasa kuna matumaini mchezeshaji huyo atakuwepo kwenye safari ya Norwich, Oktoba 19.
0 comments:
Post a Comment