KLABU ya Arsenal inamfuatilia kinda mwenye kipaji Mnigeria, Kelechi Iheanacho baada ya kufunga mabao manne dhidi ya Mexico katika mechi ya Kombe la Dunia la FIFA kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.
Iheanacho, mwenye umri wa miaka 17, anaongoza kwa mabao kwenye mashindano hayo baada ya kufanya vitu adimu dhidi ya mabingwa wa CONCACEF katika mchezo wa ufunguzi wa makundi.
Baada ya mechi, aliimbia Fifa.com: "Nimefunga mabao manne katika mechi moja kwenye mechi nyingi tu, lakini ni mitaani napocheza na rafiki zangu. Lakini haijawahi kutokea katika mechi ya kimataifa,".
Tai mdogo wa dhahabu: Kelechi Iheanacho anaing'arisha Nigeria Kombe la Dunia la 17 UAE
Kifaa: Kocha wa Arsene Wenger anaweza kumpata kinda huyo wa Nigeria
Msaka vipaji Mkuu wa Gunners, Steve Rowley yuko Falme za Kiarabu kuangalia mashindano hayo na inafahamika amevutiwa na kiwango cha kiungo huyo.
Arsenal itatakiwa kuhakikisha inamnasa kijana huyo, baada ya kuonyesha kiwango kikubwa ikiwemo kutoa pasi za mabao manne katika mechi za makundi.
VIDEO Nenda kaangalie Iheanacho alivyofunga na anavyoshangilia
Poa sana: Iheanacho akifunga katikati ya mabeki wa Mexico
0 comments:
Post a Comment