// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
ACHANA NA SAID NDEMLA, DOGO NI HABARI NYINGINE KATIKA ‘DIMBA KUBWA’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEACHANA NA SAID NDEMLA, DOGO NI HABARI NYINGINE KATIKA ‘DIMBA KUBWA’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ACHANA NA SAID NDEMLA, DOGO NI HABARI NYINGINE KATIKA ‘DIMBA KUBWA’
Na Mahmoud Zubeiry, Tanga SIMBA SC ilitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kupata sare ya 3-3 Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Baada ya mchezo huo, wataalamu wengi walisema mabadiliko yaliyofanywa na Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ mapema kipindi cha pili kuwaingiza William Lucian ‘Gallas’ na Said Hamisi Ndemla kuchukua nafasi za Haroun Chanongo na Abdulhalim Humud ndiyo yaliyoizindua Simba SC.
Said Hamisi Ndemla, kiungo hodari anayechipukia Simba SC
Naam, ni kweli kabisa. Lucian ambaye hucheza nafasi ya kiungo mkabaji na Ndemla ambaye huchezesha timu pale katikati, kwa sasa ni wachezaji muhimu mno ndani ya kikosi cha Simba SC na hazina ya taifa pia. BIN ZUBEIRY leo inamzungumzia Ndemla, kiungo chipukizi aliyepandishwa msimu huu kutoka timu ya vijana ya klabu hiyo, Simba B- kijana kwa sasa anawabeba sana Wekundu wa Msimbazi.
Said Ndemla anakaba
Anapasua kwenye misitu kama hivi
Anaambaa na mipira
Ni fundi namna hii
Ndemla jana kwa mara nyingine aliendelea kudhihirisha ubora wake wakati Simba SC ikitoka sare ya 0-0 na Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Mkwakwani kwa kucheza soka maridadi yenye kumaanisha yeye ni kiungo hodari. Anakaba, anapitia mipira, anatoa pasi nzuri, anazuia mipira, anatembea na mpira, anapiga vyenga, ni fundi na mwili wake wote unaouna mpira, kiasi kwamba anaweza kuuchezea hata kama macho hayautazami.
Anatoa pasi za kinyumenyume kama Ronaldinho wa Brazil enzi zake Barcelona
Pasi inaelekea kwa mlengwa Jonas Mkude
Mkude anapiga mpira mrefu
Hajawahi kuitwa timu ya taifa, lakini bila shaka kama ataendelea kucheza vyema katika mechi ya Jumatatu dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tarajia kocha Mdenmark, Kim Poulsen atamuita katika kikosi cha Bara kitakachokwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwezi ujao. Safu ya kiungo ya Coastal jana iliundwa na viungo wazoefu wa kimataifa wa Kenya, Jerry Santo na Crispin Odula, lakini ni sahihi kusema wote walifunikwa na Ndemla Uwanja wa Mkwakwani na picha zinazoambatana na makala hii zinathibitisha.
Hapotezi mpira hata akidondoshwa chini
Ramadhani Singano 'Messi' kulia hana wasiwasi anajua Ndemla atainuka na mpira
Na kweli, huyo anainuka nao
Anaambaa nao huku akiangalia aupeleke wapi kwa nani
Huu ni mwanzo mzuri wa kiungo huyu, lakini anahitaji uendelezwaji ili atimize ndoto zake na hilo ni jukumu la viongozi wa Simba SC, vinginevyo muda si mrefu ataingizwa kwenye kundi la akina Haroun Chanongo, kurudishwa Simba B akaboreshe kiwango. Chanongo naye alikuwa moto msimu uliopita alipopandishwa kutoka timu B, lakini wiki hii amerudishwa kikosi cha pili akaboreshe kiwango. Vijana kadhaa waliibuka vizuri kutoka Simba B siku za karibuni akiwemo Christopher Edward na Abdallah Seseme, lakini cheche zao zimepotea. Hayo ni mambo ambayo viongozi wa Simba SC wanatakiwa wayafanyie kazi- lazima kuna sehemu wanakosea katika malezi ya vijana hao. Yote kwa yote, Said Hamisi Ndemola ni habari nyingine.
Jerry Santo akimpiga teke la kinena Said Ndemla, lakini hata hakuugulia maumivu
Crispin Odula anafunga tela kwa Ndemla
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alishuhudia vitu vya Ndemla kwa mara nyingine, je wanamuendelezaje huyu kijana?
Lookman crowned African footballer of the year
-
The 2024 Confederation of African Football (CAF) Award took center stage on
Monday night, with the best talents in African football emerging winners.
The...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment