IMEWEKWA SEPTEMBA 15, 2013 SAA 2:28 ASUBUHI
KIASI cha wiki mbili tangu mashabiki wa Yanga washambulie basi la Coastal Union, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kujeruhi mmoja wa wachezaji wa timu hiyo, jana vurugu za aina hiyo zimetokea Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Basi la Yanga lilishambuliwa kwa chupa na mawe wakati linaingia Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kwa bahati nzuri aliyeumia ni dereva tu. Basi limepasuliwa kioo na mashabiki wa timu mpya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mbeya City.
Bado chupa na mawe zilikuwa zinarushwa uwanjani wakati mchezo ukiendelea.
Baada ya vurugu za kwenye mchezo wa Yanga na Coastal na Union, Kamati ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliitoza Yanga faini ya Sh. Milioni 1, yaani Sh. 500,000 kwa kila kosa, kutokana na washabiki wake kuwarushia waamuzi chupa za maji baada ya Coastal Union kusawazisha bao katika mechi hiyo na kuwarushia chupa waamuzi hao wakati wakirejea vyumbani baada ya pambano hilo.
Suala la kushambuliwa kwa basi la Coastal halikuchukuliwa hatua na sababu hazikuelezwa.
Ajabu kocha wa makipa wa Coastal Union, Juma Pondamali aliyewakejeli tu mashabiki Uwanja wa Taifa, alipewa adhabu kubwa kuliko Yanga SC, kwa kupigwa faini ya Sh. Milioni 1 na kufungiwa miezi mitatu.
Marefa waliochezesha mechi hiyo, Martin Saanya na msaidizi wake namba moja, Jesse Erasmo nao wamefungiwa mwaka mmoja kila mmoja kwa kutoimudu mechi hiyo.
Baada ya yaliyotokea katika mchezo wa Yanga na Coastal niliandika; Samaki mkunje angali mbichi na ni bora kuchukua tahadhari kabla ya hatari. TFF, imekuwa ikinyamazia matukio yenye dalili za kuleta athari kubwa zaidi mbele, jambo ambalo hakika si zuri.
Haikuwa mara ya kwanza kwa mashabiki wa Yanga kufanya fujo uwanjani na kusababisha uharibifu wa mali na hata kujeruhi na kwa ujumla kuhatarisha amani. Wenye soka yao, FIFA wanauita mchezo wa kiungwana- hawataki uhuni hata kidogo na TFF kama wasimamizi wakuu wa soka nchini, wanapaswa kulizingatia hilo.
Lakini tatizo kubwa, TFF wanashindwa kuchukua adhabu ambazo zitakuwa fundisho kwa mashabiki wa Yanga na wengine wote, kwa sababu wameweka mbele fedha kuliko utu na thamani ya mchezo wenyewe.
Nilisema, wakati umefika sasa, Yanga ipewe adhabu ya kucheza mechi bila mashabiki uwanjani, japo mechi tatu tu na bila shaka baada ya kukosa fedha, viongozi wake wataona umuhimu wa kuwasihi mashabiki wao wawe wastaarabu. Lakini kama tutaendelea na ile desturi ya faini Sh. 500,000 na kutakiwa kufidia gharama za uharibifu na tiba za waliojeruhiwa, hakika iko siku litakuja kutokea kubwa.
Nilisema, ni wazi kama tunataka kuivusha soka yetu katika hatua nyingine, lazima kwanza tukubali kujivua ushabiki na kuchukua hatua ambazo moja kwa moja zitalenga maslahi na ustawi wa mchezo huu nchini. Wakati umefika sasa, tuondoe dhana kwamba Simba na Yanga haziwezi kupewa adhabu kali, kisa ni timu kubwa na zinazalisha mapato mengi. Si sahihi.
Sasa matokeo yake na mashabiki wa mikoani nao wanaiga vurugu, tena wanazifanya kisawasawa na kuhatarisha amani kabisa. Bado najiuliza, kama mashabiki wa Yanga baada ya vurugu zote walizofanya dhidi ya Coastal, timu yao ingepewa adhabu ya kucheza bila mashabiki japo mechi moja tu, je na mashabiki wa Mbeya City jana wangefanya walichokifanya?
Mfano mdogo tu; wakati fulani mashabiki wa Ashanti walifanya vurugu katika mechi dhidi ya Yanga SC na wakafungiwa kucheza Uwanja wa Taifa na sasa timu yao imerejea Ligi Kuu wamekuwa na nidhamu ya hali ya juu, wakikumbuka adhabu waliyowahi kupata.
Yanga SC wanalaani. Wanalalamika ile mbaya vurugu walizofanyiwa na mashabiki wa Mbeya City jana, lakini viongozi wao walikaririwa na vyombo vya habari wakisema hawawezi kulaani vurugu walizofanyiwa Coastal. Hii ndiyo wanasema, mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu. Alamsiki.