• HABARI MPYA

        Tuesday, September 17, 2013

        VAN PERSIE ATAKA KUONGEZA MKATABA MAN UNITED

        IMEWEKWA SEPTEMBA 17, 2013 SAA 7:21 MCHANA
        MSHAMBULIAJI Robin van Persie anataka kuongeza mkataba wa kuichezea Manchester United ndani ya miaka yake mitatu ilyobaki katika Mkataba wake wa sasa.
        Van Persie alikuwa na mwanzo mzuri katika msimu wake wa kwanza Old Trafford, akitwaa kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu England kwa mara ya pili mfululizo na kuiwezesha United kutwaa taji Barclays.
        Inamaanisha Mholanzi huyo hakukosea kuondoka Arsenal na kuhamia kwa wapinzani wao wao.
         VIDEO  Kaangalie Manchester United wakifanya mazoezi kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa
        Flying Dutchman: Van Persie (second right) is mobbed after scoring against Crystal Palace on Saturday
        Mholanzi matawi ya juu: Van Persie (wa pili kulia) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga dhidi ya Crystal Palace Jumamosi
        Akizungumza na mshindi wa zamani wa Kombe la Ulaya na United, Paddy Crerand katika mahojiano maalum ya Televisheni ya klabu hiyo, MUTV, Van Persie alisema anataka kuendelea kuichezea zaidi klabu hiyo.
        "Nina mika mitatu zaidi mbele, ningependa kukaa zaidi,"alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. "Nafahamu, na ninaona watu walionizunguka, kufanya maamuzi ambayo nafikiri hao watu wanaweza kugeuka na kusema; "Yalikuwa ni mazuri?". Sitaki hivyo.
        "Nataka kucheza muda mrefu kadiri inavyowezekana katika kiwango cha juu,".
        Kushinda mataji ndio kitu kinachomvutia zaidi Van Persie, ambaye hakuwahi kushinda chochote akiwa Arsenal tangu walipotwaa Kombe la FA kwa kuifunga United kwenye Fainali mwaka 2005.
        Champions: Van Persie celebrates winning the Premier League title back in May
        Bingwa: Van Persie akisherehekea kushinda ubingwa wa Ligi Kuu, Mei mwaka huu
        Tayari ameongeza taji la Ngao ya Jamii katika kabati lake baada ya ubingwa wa Ligi Kuu na ana matumaini ya kunyanyua mataji zaidi United.
        "Hiyo (kushinda mataji) ndiyo mpango mzima,"alisema. "Mwaka jana tulipata taji moja kati ya manne. Sasa tunatakiwa kutazama hili katika upande mwingine.
        "Tuna nafasi ya kupata matano mwaka huu. Mangapi tutabeba kati ya hayo matano? Kwa mtazamo wangu tutakuwa tayari kushinda mawili au matatu.'
        Baada ya mechi mbili bila ushindi wala bao, United walirejea kwenye furaha ya ushindi katika Ligi Kuu England mwishoni mwa wiki, huku Van Persie akifunga bao lake la tano msimu huu katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace waliomaliza 10.
        Moving on: Van Persie joined United last summer from Arsenal
        Endelea: Van Persie alitua United msimu uliopita kutoka Arsenal
        Sasa Mashetani Wekundu wanaingia katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa katika zama za David Moyes, wakimenyana na Bayer Leverkusen usiku wa leo.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: VAN PERSIE ATAKA KUONGEZA MKATABA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry