// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ULIMWENGU APIGA MBILI, SAMATTA MOJA NA PASI YA BAO TP MAZEMBE IKIUA 4-2 NA KUTINGA NUSU FAINALI AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ULIMWENGU APIGA MBILI, SAMATTA MOJA NA PASI YA BAO TP MAZEMBE IKIUA 4-2 NA KUTINGA NUSU FAINALI AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 15, 2013

    ULIMWENGU APIGA MBILI, SAMATTA MOJA NA PASI YA BAO TP MAZEMBE IKIUA 4-2 NA KUTINGA NUSU FAINALI AFRIKA

    Na Prince akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 15, 2013 SAA 9:07 ALASIRI
    WASHAMBULIAJI wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu jana kwa pamoja walifunga mabao matatu wakati TP Mazembe ikiifunga Entente Setif ya Algeria 4-2 mjini Lubumbashi na kutinga Nusu Fainail ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Thomas Ulimwengu alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na Samatta moja, wakati linguine lilifungwa na Tressor Mputu Mabi.
    Ulimwengu aliifungia Mazembe bao la kwanza dakika ya nne kwa kichwa, ambalo halikudumu sana baada ya beki Mohamed Ziti kusawazisha dakika nne baadaye.
    Watau hatari; Kutoka kulia ulimwengu, Mputu na Samatta jana

    Mazembe ikazinduka na kupata bao la pili dakika ya 16 lililofungwa na Tessor Mputu, ambaye aliipangua safu ya ulinzi ya Setif na kumtungua kipa Sofiane Khedairia.
    Ulimwengu akaifungia Mazembe la tatu dakika ya 27, akimalizia krosi maridadi ya Mbwana Samatta, ambaye alimtoka Abdelghani Demmou.
    Jinsi Mbwana Samatta anavyopendwa Mazembe
    Mazembe ilipata bao la nne dakika ya nne baada ya kutimia saa moja mchezoni kupitia kwa Samatta, ambaye alitumia vizuri udhaifu wa beki Demmou.
    Samatta akimiliki mpira mbele ya beki wa Setif
    Ulimwengu akitafuta njia ya kuchomokea

    Tressor Mputu akitafuta mbinu za kumtoka mtu
    Mputu alipata nafasi nzuri ya kufunga dakika tatu baadaye, lakini Khedaria akaokoa na Setif ikapata bao linguine dakika ya 71 kupitia kwa mshambuliaji wake, Kaled Gourmi, aliyemtungua vizuri kipa Robert Kidiaba.
    Mazembe ilipewa penalti dakika za majeruhi, lakini kiungo Ngasanya Ilongo akapaisha.

    Samatta akipambana katika mchezo wa jana

    Samatta akivizia mpira udondoke afanye mambo

    Stopila Sunzu anakaba

    Robert Kidiaba akiwa amedaka
    Timu hiyo ya DRC sasa imetinga Nusu Fainali ikiwa bado ina mchezo mmoja mkononi, baada ya kutimiza pointi 10 kutokana na mechi tano.
    FUS Rabat, ambayo itamaliza na Mazembe katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo B, inaweza kuungana na akina Samatta na Ulimwengu ikiwa itawafunga wenyeji CA Bizertin ugenini Tunisia leo. Bizertin na FUS zimefungana kwa pointi tano kikla moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ULIMWENGU APIGA MBILI, SAMATTA MOJA NA PASI YA BAO TP MAZEMBE IKIUA 4-2 NA KUTINGA NUSU FAINALI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top