IMEWEKWA SEPTEMA 28, 2013 SAA 12:45 JIONI
BAO la Nahodha John Terry dakika ya 65 limeinusuru Chelsea kulala mbele ya Tottenham baada ya sare ya 1-1.
Timu zote zinafundishwa na makocha Wareno, Andre Villas-Boas wa Spurs na Jose Mourinho wa Chelsea.
Tottenham ilitawaa kipindi cha kwanza na kupata bao la kuongoza kupitia kwa Gylfi Sigurdsson dakika ya 20.
Kikosi cha Spurs kilikuwa: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton, Paulinho, Dembele, Townsend/Chadli dk62, Eriksen/Holtby dk69, Sigurdsson, Soldado/Defoe dk76.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Terry, Cole, Mikel/Mata dk46, Lampard, Ramires, Oscar/Azpilicueta dk82, Hazard/Schurrle dk69, Torres.
La kusawazisha: John Terry ishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kusawazisha
Kichwa: Terry akipiga kichwa kuunganisha mpira wa adhabu wa Juan Mata
La kwanza: Gylfi Sigurdsson akiteleza kufunga bao la kuongoza la Tottenham
Mtu muhimu: Sigurdsson akiondoka kushangilia baada ya kufunga Uwanja wa White Hart Lane
Sigurdsson akishangilia mbele ya mashabiki na wenzake
Ubabe: Fernando Torres akionyeshana ubabe na Jan Vertonghen, kabla ya Mspanyola huyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu
Nyekundu ya Torres, nje
Ndiyo mpira: Kocha wa Tottenham, Andre Villas Boas (kulia) akielekea kumsalimia kocha wa Chelsea, Jose Mourinho
Andros Townsend akipasua katikati ya Ashley Cole (kushoto) na Oscar