IMEWEKWA SEPTEMBA 29, 2013 SAA 3:50 USIKU
MSHAMBULIAJI Luis Suarez amerejea na moto katika Ligi Kuu ya England baada ya kumaliza adhabu yake ya mechi 10, leo akifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 wa Liverpool dhidi ya Sunderland.
Ntyota huyo wa Uruguay alifunga mabao yake katika dakika za 36 na 89 wakati lingine lilifungwa na mshambuliaji pacha wake, Daniel Sturridge dakika ya 28 na kufutia machozi la wenyeji lifungwa na Emanuele Giaccherini dakika ya 52.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet, Toure, Skrtel, Sakho, Henderson, Gerrard, Lucas, Jose Enrique, Moses/Sterling dk75, Sturridge na Suarez.
Sunderland: Westwood, Gardner, O'Shea, Cuellar, Colback, Larsson/Mavrias dk85, Cattermole/Celustka dk74, Ki,Johnson, Altidore na Giaccherini.
Baba wa familia: Luis Suarez akishangilia kwa kuonyesha picha ya mkewe na binti yake na mtoto wake mpya wa kiume, Benjamin
Amerudi na moto: Suarez amefunga kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza adhabu
Suarez akiifungia timu yake bao la pili
Daniel Sturridge alifunga bao la kwanza
Sturridge akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza
Sturridge akishangilia bao lake la saba msimu huu
Victor Moses akigombea mpura na Jack Colback
Martin Skrtel akimaa miguuni Jozy Altidore
Altidore akipambana na Kolo Toure