Na Mahmoud Zubeiry, Mbeya, IMEWEKWA SEPTEMBA 16, 2013 SAA 2:16 ASUBUHI
JKT Ruvu ndiyo timu yenye asilimia 100 ya ushindi hadi sasa baada ya mizunguko mitatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakati mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita, Kipre Herman Tchetche wa Azam raia wa Ivory Coast hadi sasa hajafunga bao hata moja, huku mshambuliaji wa Yanga SC, Jerry Tegete akiingia kwenye mbio za kuwania kurithi ‘kiatu cha dhahabu’.
JKT Ruvu inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zate tisa baada ya kushinda mechi zake zote tatu za awali hadi sasa, wakati Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wakiwa kwenye nafasi ya pili kwa pointi zao saba.
Hali bado si nzuri kwa vinara wa Ligi Kuu msimu uliopita, mabingwa Yanga SC na washindi wa pili, Azam FC hadi sasa kila timu ikiwa imevuna pointi tano baada ya mechi tatu.
Angalau Azam wanaweza kuwa na kisingizio cha kucheza mechi zote ugenini, lakini Yanga SC katika mechi hizo ni moja tu imecheza ugenini dhidi ya Mbeya City Jumamosi.
Coastal Union iliyosajili vizuri zaidi msimu huu, licha ya kuanza na ushindi wa ugenini dhidi ya JKT Oljoro na kutoa mikwara mingi, imegundulika ilikuwa nguvu ya soda baada ya Jumamosi kulazimishwa sare ya bila kufungana nyumbani na vibonde, Prisons.
Hali mbaya kwa Ashanti United, ambayo baada ya mechi tatu za awali inakuwa timu pekee ambayo haijavuna hata pointi moja- maana yake inaelekea kuendeleza desturi yake ya kupanda na kushuka Ligi Kuu.
JKT Oljoro na Prisons zimetengeneza ‘uswahiba’ na Ashanti baada ya kuvuna pointi moja kila timu katika mechi tatu. Oljoro iliyokuwa tishio wakati inapanda Ligi Kuu mwaka juzi kiasi cha kuongoza ligi hiyo mzunguko wote wa kwanza, makali yake yanaenda yakipungua na inawezekana huu ukawa msimu wao wa mwisho katika ligi hiyo.
Oljoro inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imecheza mechi zote za awali nyumbani Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha lakini imeambulia pointi moja kwa sare na Rhino Rangers baada ya kufungwa na Coastal Union na Simba SC.
Kwa upande wa mbio za kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu, Kipre Tchetche amefikisha mechi tatu bila kufunga bao hata moja.
Hakuna mchezaji aliyefunga zaidi ya mabao mawili hadi sasa na wachezaji sita Jerry Tegete, Didier Kavumbangu, wote wa Yanga SC, Jonas Mkude wa Simba SC, Elias Maguri wa Ruvu Shooting, Bakari Kondo wa JKT Ruvu na Saad Kipanga wa Rhino Rangers wamefungana kwa mabao mawili kila mmoja baada ya mechi tatu.
Kati ya hao ni Jonas Mkude pekee aliyefunga kwa penalti bao lake moja.
Ligi Kuu itaingia katika mzunguko wake wa nne keshokutwa, mabingwa watetezi, Yanga SC wakirejea Uwanja wa Sokoine, Mbeya kumenyana na Prisons.
Simba SC itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar itaikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Azam FC na Ashanti United Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Coastal Union na Rhino Rangers Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mtibwa Sugar na Mbeya City Uwanja wa Manungu, Morogoro na Ruvu Shootings dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Mabatini, Pwani.
JKT Ruvu inaweza kusimamishwa na Ruvu Shooting Jumatano Mabatini- maana yake Simba SC ina nafasi ya kupanda kileleni kwa mara ya kwanza msimu huu ikiifunga Mgambo JKT keshokutwa. Kumbuka, naitwa Mahmoud, ukipenda niite Bin Zubeiry. Asante kwa kusoma rafiki. Endelea kusoma bongostaz.blogspot.com, hutaichoka.

Vinara; JKT Ruvu asilimia 100 |

Mabao yamekauka; Mfungaji bora Kipre Tchetche amecheza mechi tatu bila kufunga bao |
JKT Oljoro na Prisons zimetengeneza ‘uswahiba’ na Ashanti baada ya kuvuna pointi moja kila timu katika mechi tatu. Oljoro iliyokuwa tishio wakati inapanda Ligi Kuu mwaka juzi kiasi cha kuongoza ligi hiyo mzunguko wote wa kwanza, makali yake yanaenda yakipungua na inawezekana huu ukawa msimu wao wa mwisho katika ligi hiyo.
Oljoro inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imecheza mechi zote za awali nyumbani Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha lakini imeambulia pointi moja kwa sare na Rhino Rangers baada ya kufungwa na Coastal Union na Simba SC.
Kwa upande wa mbio za kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu, Kipre Tchetche amefikisha mechi tatu bila kufunga bao hata moja.
Ameanza vizuri; Didier Kavumbangu ana mabao mawili baada ya mechi tatu |
Hakuna mchezaji aliyefunga zaidi ya mabao mawili hadi sasa na wachezaji sita Jerry Tegete, Didier Kavumbangu, wote wa Yanga SC, Jonas Mkude wa Simba SC, Elias Maguri wa Ruvu Shooting, Bakari Kondo wa JKT Ruvu na Saad Kipanga wa Rhino Rangers wamefungana kwa mabao mawili kila mmoja baada ya mechi tatu.
Kati ya hao ni Jonas Mkude pekee aliyefunga kwa penalti bao lake moja.
Ligi Kuu itaingia katika mzunguko wake wa nne keshokutwa, mabingwa watetezi, Yanga SC wakirejea Uwanja wa Sokoine, Mbeya kumenyana na Prisons.
Simba SC itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar itaikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Azam FC na Ashanti United Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Coastal Union na Rhino Rangers Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mtibwa Sugar na Mbeya City Uwanja wa Manungu, Morogoro na Ruvu Shootings dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Watapanda kileleni Jumatano? Simba wanaweza kupanda kileleni Jumatano wakiifunga Mgambo na JKT Ruvu wakafungwa na Ruvu Shooting |
JKT Ruvu inaweza kusimamishwa na Ruvu Shooting Jumatano Mabatini- maana yake Simba SC ina nafasi ya kupanda kileleni kwa mara ya kwanza msimu huu ikiifunga Mgambo JKT keshokutwa. Kumbuka, naitwa Mahmoud, ukipenda niite Bin Zubeiry. Asante kwa kusoma rafiki. Endelea kusoma bongostaz.blogspot.com, hutaichoka.
MSIMAMO | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | |
1 | JKT Ruvu | 3 | 3 | 0 | 0 | 6 | 0 | 6 | 9 |
2 | Simba SC | 3 | 2 | 1 | 0 | 5 | 2 | 3 | 7 |
3 | Ruvu Shooting | 3 | 2 | 0 | 1 | 5 | 2 | 3 | 6 |
4 | Yanga SC | 3 | 1 | 2 | 0 | 7 | 3 | 4 | 5 |
5 | Azam FC | 3 | 1 | 2 | 0 | 7 | 3 | 4 | 5 |
6 | Coastal Union | 3 | 1 | 2 | 0 | 3 | 1 | 2 | 5 |
7 | Mbeya City | 3 | 1 | 2 | 0 | 3 | 2 | 1 | 5 |
8 | Mtibwa Sugar | 3 | 1 | 1 | 1 | 2 | 3 | -1 | 4 |
9 | JKT Mgambo | 3 | 1 | 0 | 2 | 1 | 3 | -2 | 3 |
10 | Kagera Sugar | 3 | 0 | 2 | 1 | 1 | 2 | -1 | 2 |
11 | Rhino Rangers | 3 | 0 | 2 | 1 | 3 | 5 | -2 | 2 |
12 | JKT Oljoro | 3 | 0 | 1 | 2 | 1 | 4 | -3 | 1 |
13 | Tanzania Prisons | 3 | 0 | 1 | 2 | 0 | 6 | -6 | 1 |
14 | Ashanti United | 3 | 0 | 0 | 3 | 1 | 7 | -6 | 0 |