// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ROONEY HATARINI KUWAKOSA LIVERPOOL LEO, AUMIA KICHWA MAZOEZINI NA KUFUNGWA BANDEJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ROONEY HATARINI KUWAKOSA LIVERPOOL LEO, AUMIA KICHWA MAZOEZINI NA KUFUNGWA BANDEJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Sunday, September 01, 2013

        ROONEY HATARINI KUWAKOSA LIVERPOOL LEO, AUMIA KICHWA MAZOEZINI NA KUFUNGWA BANDEJI

        IMEWEKWA SEPTEMBA 1, 2013 SAA 11:14 ALFAJIRI
        MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amezalisha hofu Manchester United baada ya kuumia kichwa jana asubuhi na sasa kuna wasiwasi akaukosa mchezo wa leo dhidi ya Liverpool.
        Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England aliumia kichwa mazoezini asubuhi na aliondoka Uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, Carrington HQ akiwa amefungwa bandeji iliyozunguka kichwa.
        Committed: Waynre Rooney (right) challenges Ashley Cole after coming on as substitute in Monday's 0-0 draw with Chelsea
        Ameumia: Wayne Rooney (kulia) akipambana na Ashley Cole katika mchezo dhidi ya Chelsea JUmatatu

        Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yuko shakani sasa kucheza Anfield leo na hatima yake itaamuliwa na madaktari wa timu hiyo.
        Rooney alicheza soka ya nguvu United ikimenyana na Chelsea Jumatatu na kuondoa shaka juu ya mustakabali wake Old Trafford.
        Selection problem: David Moyes' team selection has been hit by Rooney's head injury
        Kichwa kinamuuma: Kocha David Moyes amepata pigo kwa Rooney kuumia kichwa

        Baada ya mechi hiyo, kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alimtaka mshambuliaji huyo kuweka wazi ndani ya saa 48 kama anabaki au anataka kuondoka, lakini Rooney alijibu kwa kuweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook amefurahishwa na mapokezi aliyopewa na mashabiki katika mchezo huo.
        Fans' favourite: The Old Trafford faithful applauded Rooney after the Chelsea game for his display
        Kipenzi cha mashabiki: Rooney amefurahia mapokezi ya mashabiki Old Trafford katika mechi na Chelsea

        Sasa mkonwe Ryan Giggs anaweza kuchukua nafasi ya Rooney katika mchezo wa leo, akicheza sambamba na Danny Welbeck na Robin van Persie katika safu ya ushambuliaji. Mchezaji anayetakiwa na Tottenham, Javier Hernandez pia amekuwa akifanya mazoezi.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: ROONEY HATARINI KUWAKOSA LIVERPOOL LEO, AUMIA KICHWA MAZOEZINI NA KUFUNGWA BANDEJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry