IMEWEKWA SEPTEMBA 15, 2013 SAA 11:21 JIONI
MRENO Cristiano Ronaldo amesaini Mkataba mnono wa miaka mitano kuendelea kuichezea Real Madrid, wenye thamani ya Pauni Milioni 76 (zaidi ya Euro Milioni 90) inayomfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani na amesema anataka kustaafu soka yake Madrid.
Ronaldo amesaini Mkataba huo Santiago Bernabeu leo na rais wa klabu, Florentino Perez siku moja baada ya kufunga Madrid ikitoa sare ya 2-2 na Villarreal.
Kiwango hicho kinamfanya awe analipwa karibu mara mbili ya malipo ya Gareth Bale na kinarejesha heshima yake baada ya kupoteza hadhi ya mwanasoka ghali duniani, kufuatia Real kumnunua Bale kwa Pauni Milioni 86.
VIDEO Kaangalie mchezaji anayelipwa Pauni Milioni 76 Ronaldo akifanya mazoezi na wenzake Real Madrid
Dole tupu: Cristiano Ronaldo akiwa na Rais Florentino Perez baada ya sherehe za kuutangaza Mkataba wake mpya Santiago Bernabeu
Haendi popote: Ronaldo akiwa Santiago Bernabeu kusaini Mkataba mpya
Mambo yamekuwa: Ronaldo akiwa na Rais Florentino Perez baada ya kusaini Mkataba mpya
Katika mkataba huo mpya, Real itamlipa Ronaldo Pauni Milioni 15 kwa mwaka baada ya makato ya kodi na nje ya posho mbalimbali. Bale analipwa Pauni Milioni 8.3 kwa msimu na mshahara mpya wa Ronaldo unamfanya azidi kwa Pauni 850,000 kwa mwaka, mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic.
Pia inazima kabisa ndoto za klabu yake ya zamani Manchester United kumrejesha Ronaldo Old Trafford.
"Nina furaha haswa hapa,"alisema. "Nitakuwa hapa kwa miaka mitano zaidi. Nataka kushinda mataji katika klabu hii.
Mkataba mpya: Cristiano Ronaldo amesaini Mkataba mpya mnono Real Madrid
Mkataba wa Real: Ronaldo amesema anataka kumalizia soka yake Madrid
Wote wanatabasamu: Ronaldo akizungumza na vyombo vya Habari Hispania baada ya kusaini Mkataba mpya
"Nawakubali mashabiki wanavyonipenda hapa. Nina furaha, nataka kuonyesha mavitu yangu uwanjani. Nitakuwa mkweli kwako- kila mmoja anajua nilikuwa Manchester kwa miaka sita. Manchester ni ya kale sasa. Sasa klabu yangu ni Real Madrid. Hii ni nyumbani, familia yangu iko hapa na nina furaha haswa hapa.
"Naziheshimu klabu zote zilizonitaka. Lakini wakati wote wanafahamu uamuzi wangu, kwamba lengo langu ni kuwa hapa na kucheza labda, pengine, mwisho wa maisha ya soka. "Yajayo hakuna ajuaye,".