IMEWEKWA SEPTEMBA 18, 2013 SAA 7:07 USIKU
NYOTA Gareth Bale ametokea benchi na kupikia mabao mawili Real Madrid ikiitandika Galatasaray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake ya 21 Bernabeu.
NYOTA Gareth Bale ametokea benchi na kupikia mabao mawili Real Madrid ikiitandika Galatasaray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake ya 21 Bernabeu.
Bale aliwashuhudia Isco, Karim Benzema na Ronaldo wakiiweka klabu yake mbele kwa mabao 3-0 kabla ya kuingia na kutoa mchango wake kunenepesha ushindi.
Kwanza, ilikuwa mpira wa adhabu wa winga huyo wa Wales uliomkuta Ronaldo, ambaye akaifungia bao la nne timu ya Carlo Ancelotti. Kisha akampa pasi Ronaldo, ambaye alimpasia pia Benzema kabla ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo.
Isco alifunga dakika ya 33, Benzema 54 na 81 Ronaldo 63, 66 na 90, wakati bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Bulut dakika ya 84.
Didier Drogba alicheza kwa dakika 45 tu kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Amrabat.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas/Lopez dk14, Carvajal, Ramos, Pepe, Arbeloa, Modric/Illarramendi dk72, Khedira, Di Maria, Isco/Bale dk64, Ronaldo na Benzema
Galatasaray: Muslera, Eboue, Chedjou, Nounkeu, Riera, Inan, Melo, Baytar/Bruma dk62, Yilmaz, Sneijder na Drogba/Amrabat dk46.

Anaondoka na mpira wake: Cristiano Ronaldo akiwa ameweka mpira kwenye jezi yake baada ya kufunga Hat-trick mjini Istanbul
MATOKEO KAMILI NA WAFUNGAJI LIGI YA MABINGWA:
|
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|
Kazi nzuri: Cristiano Ronaldo akikumbatiana na Gareth Bale baada ya kufunga bao lake la pili
Mchezaji ghali duniani...anatokea benchi: Bale aliingia kipindi cha pili kuisaidia Real Madrid kuisambaratisha Galatasaray
Wawili ghali: Gareth Bale (kulia) akiongozana na Cristiano Ronaldo wakati akishangilia bao lake la pili
ameenda hewani: Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake la kwanza
Kazi nzuri: Karim Benzema akishangilia bao lake
Kimya kimya: Isco alifunga bao la kwanza
Hasira: Cristiano Ronaldo akimlalamikia refa baada ya kuangushwa
Benchi: Gareth Bale akiangalia mechi kutokea benchi kipindi cha kwanza kabla ya kuingia na kufanya kazi nzuri