IMEWEKWA SEPTEMBA 30, 2013 SAA 6:52 USIKU
KUELEKEA Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki hii, mechi za hatua ya makundi, BIN ZUBEIRY inakuletea tathmini kwa ufupi juu ya zitakazomenyana na timu za Uingereza.
Steaua Bucharest v Chelsea
Kundi E: Jumanne Saa 3.45 usiku
Steaua imepaa kileleni kwa pionti tatu zaidi katika Ligi Kuu ya Romania, baada ya kuilaza Poli Timisoara mabao 3-0, ambayo yalitiwa kimiani na Federico Piovaccari, Nicolae Stanciu na Adrian Popa.
Arsenal v Napoli
Kundi F: Jumanne Saa 3.45 usiku
Mabao mawili ya Goran Pandev yameipa Napoli pointi tatu dhidi ya Genoa na kupaa kileleni mwa Ligi Kuu Italia, Serie A. Wanalingana kwa pointi na Juventus, 16 kila timu baada ya mechi sita, lakini wanashika usukani kwa wastani wao mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Tunateleza: Napoli ilifungua akaunti yake ya Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa 2-1 dhidi washindi wa pili wamsimu uliopita, Dortmund
Celtic v Barcelona
Kundi H: Jumanne Saa 3.45 usiku
Lionel Messi ataikosa mechi hiyo na kuwa nje kwa wiki tatu nyingine, baada ya kuumia nyama za mguu wake wa kulia.
Mwanasoka huyo bora wa dunia alitolewa wakati timu yake ikhinda 2-0 dhidi ya Almeria Jumamosi muda mfupi tu baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 21, ambalo lilikuwa bao lake la nane msimu huu.
Atakosekana: Messi atakuwa nje kwa wiki tatu kutokana na maumivu ya nyama, aliyoyapata katika mechi kati ya Barcelona na Almeria
Manchester City v Bayern Munich
Kundi D: Jumatano Saa 3.45 usiku
Thomas Muller alifunga bao pekee katika mchezo mgumu wakati Bayern Munich ikiifunga Wolfsburg 1-0 na kuendelea kukabana koo na Dortmund kileleni mwa Bundesliga. Wana pointi 19 baada ya mechi saba bila kufungwa hata moja.
Urejeo: Shakhtar, iliyoifunga Real Sociedad katika mechi za kwanza, ililazimishwa sare mwishoni mwa wiki
Shakhtar Donetsk v Manchester United
Kundi A: Jumatano Saa 3.45 usiku
Shakhtar imepanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ukraine, baada ya Eduardo kuwafungia bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Metalurh.
Walikuwa wamekwishalala 2-0 lakini walirudisha moja kupitia kwa Alex Teixeira dakika ya 54 na wakajipatia pointi moja, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal kusawazisha zikiwa zimesalia dakika nane.