Na Mahmoud Zubeiry, Mbeya, IMEWEKWA SEPTEMBA 16, 2013 SAA 1:15 ASUBUHI
KOCHA Mkuu wa timu ya Mbeya City ya hapa, Juma Mwambusi amesema kwamba kocha Mholanzi wa Yanga SC, Ernie Brandts ameshindwa kuiunganisha timu hiyo kuweza kucheza kitimu hadi sasa na hilo ndilo tatizo kubwa kwenye kikosi chake kwa sasa.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY mjini hapa, Mwambusi alisema mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wana wachezaji wazuri, lakini tatizo kubwa hawachezi kitimu, bali wanacheza kwa uwezo binafsi wa kila mchezaji.
“Unajua tatizo ambalo nimeliona Yanga SC ni kwamba wana wachezaji wapya kwenye timu yao, sasa huyu mwalimu nadhani bado hajawaunganisha waweze kucheza timu, anatakiwa kuharakisha kuiunganisha timu icheze kitimu,”alisema.
Hata hivyo, Mwambusi alisema bado ana matumaini sana na Yanga SC kwamba inaweza kutetea ubingwa wake, kwa kuwa ina wachezaji wazuri, bali tu Brandts anatakiwa kufanya kazi ya ziada kuiunganisha timu.
Kuhusu malalamiko ya Yanga SC kwamba walitoa sare ya 1-1 na Mbeya City kwa sababu ya kucheza kwenye Uwanja mbovu wa Sokoine, Mwambusi alisema; “Si kweli, timu zote Tanzania zinafanya mazoezi kwenye viwanja vibovu pengine kuliko hata ule wa Sokoine,”.
Mwambusi aliwashauri Yanga kuachana na visingizio wanapofanya vibaya, bali wafanyie kazi mapungufu yao ili kurekebisha makosa katika timu yao na ndiyo itawasaidia.
Akiizungumzia timu yake ambayo pamoja na kucheza mechi tatu za awali za Ligi Kuu nyumbani imeambulia ushindi mmoja na sare mbili, Mwambusi alisema; “Si mbaya, kwa kuwa timu yangu ni mpya katika Ligi Kuu, na tumecheza zote ngumu, Yanga ni mabingwa na Kagera Sugar pia ni timu nzuri na hata Ruvu Shooting ni wazuri pia,”alisema.
Mbeya imetoa sare na Yanga na Kagera na kuifunga Ruvu na jana imeondoka hapa kwenda Manungu, Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar Jumatano.
“Hatuna wasiwasi na mechi za ugenini, sisi hata kupanda kwetu Ligi Kuu tulicheza mechi nyingi sana ugenini. Na baada ya kupanda, pia tumecheza mechi nyingi za kuijipima nguvu ugenini, hivyo tunakwenda kuanza mechi za ugenini tukiwa na matumaini ya kufanya vizuri,”alisema Mwambusi, kipenzi cha wana Mbeya.

Hawachezi kitimu; Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amewashauri Yanga SC kuboresha timu yao |
“Unajua tatizo ambalo nimeliona Yanga SC ni kwamba wana wachezaji wapya kwenye timu yao, sasa huyu mwalimu nadhani bado hajawaunganisha waweze kucheza timu, anatakiwa kuharakisha kuiunganisha timu icheze kitimu,”alisema.
Hata hivyo, Mwambusi alisema bado ana matumaini sana na Yanga SC kwamba inaweza kutetea ubingwa wake, kwa kuwa ina wachezaji wazuri, bali tu Brandts anatakiwa kufanya kazi ya ziada kuiunganisha timu.
Wachezaji wazuri, lakini hawajaunganishwa; Yanga SC na Mbeya City Jumamosi Uwanja wa Sokoine |
Hussein Javu wa Yanga SC akipambana na wachezaji wa Mbeya City kugombea mpira Jumamosi |
Kuhusu malalamiko ya Yanga SC kwamba walitoa sare ya 1-1 na Mbeya City kwa sababu ya kucheza kwenye Uwanja mbovu wa Sokoine, Mwambusi alisema; “Si kweli, timu zote Tanzania zinafanya mazoezi kwenye viwanja vibovu pengine kuliko hata ule wa Sokoine,”.
Mwambusi aliwashauri Yanga kuachana na visingizio wanapofanya vibaya, bali wafanyie kazi mapungufu yao ili kurekebisha makosa katika timu yao na ndiyo itawasaidia.
Mabosi walijionea; Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji (kushoto), akiwa na Makamu wake, Clement Sanga na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mussa Katabaro. |