IMEWEKWA SEPTEMBA 30, 2013 SAA 10:37 JIONI
WACHEZAJI wa Crystal Palace, Marouane Chamakh na Dean Moxey ilibidi watenganishwe na wachezaji wenzao baada ya kugombana katika chumba cha kubadilishia nguo Jumamosi wakicheza na Southampton.
Ugomvi huo ulifuatia kipigo cha mabao walichopewa Palace cha maao 2-0 – ambacho ni cha sita katika mechi sabaza Ligi Kuu England msimu huu – kinachoifanya timu hiyo ya Ian Holloway ishike nafasi ya pili kutoka mkiani.
Haifahamiki chanzo cha ugomzi wao, lakini Holloway hakufurahishwa na kitendo cha Chamakh, baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal kuonyeshwa kadi kwa kujirusha Uwanja wa St Mary’s kipindi cha kwanza.
Wanawakiana: Marouane Chamakh akifokeana na Dean Moxey, ugomi ambao uliendelea hadi chumba chao cha kubadilishia nguo
Palace iliombwa kuzungumzia tukio hilo, lakini ilikataa.
Chamakh alifika karibu na lango la wapinzani dakika ya 27 Uwanja wa St Mary's na akajirusha ili kusaka penalti ingawa angeweza kupiga shuti kujaribu kufunga.
Baada ya hapo walijizibizana na Moxey uwanjani wakati mchezo ukiendelea, ugomvi kumbe uliendelea hadi chumbani.
Ilibaki kuchapana tu: Chamakh na Moxey waliwakiana sana Uwanja wa St Mary's
Kujirusha? Chamakh alipewa kadi kwa kujiangusha akiwa kwenye nafasi ya kufunga
Muongo? Kocha wa Palace, Holloway pia hakufurahishwa na kitendo hiki
Aliguswa? Palace hawakupewa penalti Chamakh alipoanguka
Hasira: Chamakh akionyeshwa kadi ya njano kwa kujiangusha
Mchezaji mpya: Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Chamakh amejiunga na Palace majira haya ya joto