IMEWEKWA SEPTEMBA 15, 2013 SAA 2:55 ASUBUHI
BONDIA Floyd Mayweather Jnr amempiga kiulaini kwa pointi mpinzani wake, Saul 'Canelo' Alfvarez katika pambano lililomalizika hivi karibuni ukumbi wa MGM Grand mjini Las Vegas, Marekani.
Jaji mmoja tu alitoa sare pambano hilo, lakini wengine wawili walimpa ushindi Mayweather katika pambano hilo la Raundi 12.
Jaji CJ Ross alichekesha kutoa pointi 114-114 wakati Dave Moretti alimpa Mayweather 116-112 na Craig Metcalfe, akampa 117-11 na Alvarez alipigwa raundi zote.
Bado bingwa: Floyd Mayweather alitamba sana na kumshinda kiulaini Saul Alvarez
Mtu anapewa kichapo: Floyd Mayweather akimchapa Saul Alvarez
Floyd Mayweather alimpiga Saul Alvarez Raundi zote 12
Alvarez akiwa anatia huruma
RAUNDI KWA RAUNDI NA JEFF POWELL
Mayweather | Raundi | Alvarez |
---|---|---|
10 | 1 | 9 |
10 | 2 | 9 |
10 | 3 | 9 |
10 | 4 | 9 |
10 | 5 | 9 |
10 | 6 | 9 |
10 | 7 | 9 |
10 | 8 | 9 |
10 | 9 | 9 |
10 | 10 | 9 |
10 | 11 | 9 |
10 | 12 | 9 |
120 | Total | 108 |
Las Vegas ni nyumbani kwa kuhamia kwa Mayweather, lakini wengi kati ya watu 17,000 waliokuwapo kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena walikuwa wa Mexico anatokea mpinzani wake.
Walifika kwa wingi kumsapoti bondia wao na kushereheka siku ya Uhuru wao. Walikuwa wakipiga kelele ukumbi mzima, lakini Mayweather alisimama imara.
Mayweather si tu ni bingwa wa mataji yote ya uzito wa Light-Middle duniani, lakini pia ni bondia bora kabisa zama hizi.
Alvarez alizidiwa mno Mayweather na kukubali kupewa makonde mengi, hivyo kumaliza pamba akiwa hoi.
Mayweather anamuadhibu Alvarez
Mayweather alimfanya vibaya Alvarez
Alvarez ngumi zake nyingi hazikumpata Mayweather
Alvarez akisota japo kufikisha ngumi kifuani kwa Mayweather
Angalau amekula mbavu
Hiyo imepanguliwa
Alvarez akipewa kitu na Mayweather
Refa Kenny Bayless akimuonya Alvarez
Mayweather noma
Floyd Mayweather Sr akizungumza na mwanawe kwenye kona wakati akijiandaa kuingia Raundi nyingine
Alvarez akiwa hoi kwenye kona yake
Alvarez akielekea ulingoni na kushangilia na maelfu ya Wamexico walikuwapo
Mayweather, akipanda ulingoni katika staili ya rapa Lil Wayne
Mfalme wa ulingo: Mayweather akiwa na Justin Bieber baada ya pambano