IMEWEKWA SEPTEMBA 26, 2013 SAA 6:01 USIKU
MACHO yote yalikuwa kwa Luis Suarez baada ya kurejea Liverpool kufuatia kumaliza adhabu yake ya mechi 10, lakini Javier Hernandez akaiteka shoo kwa bao lake pekee lililoipeleka Manchester United Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One.
Hatimaye Suarez alicheza mechi yake ya kwanza ya msimu mpya baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic msimu uliopita.
Na wakati mshambuliaji huyo wa Uruguay alizomewa na mashabiki Uwanja wa Old Trafford, alikuwa ni Chicharito aliyepoza maumivu ya David Moyes kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa wapinzani, Manchester City katika Ligi Kuu Jumapili.
Liverpool ilitawa sehemu kubwa ya mchezo na Daniel Sturridge alipoteza nafasi kadhaa nzu za kufunga, lakini Hernandez hakufanya makosa alipopata nafasi dakika ya 46.
Wayne Rooney, ambaye ndiye mchezaji bora zaidi kwa United hivi sasa, alipiga kona nzuri baada ya mapumziko na Hernandez akaunganisha nyavuni.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael Da Silva, Smalling, Evans, Buttner, Jones, Giggs, Nani, Rooney, Kagawa na Hernandez.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael Da Silva, Smalling, Evans, Buttner, Jones, Giggs, Nani, Rooney, Kagawa na Hernandez.
Liverpool: Mignolet, Toure, Skrtel, Sakho, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Henderson, Suarez na Moses, Sturridge.
Shujaa: Javier Hernandez akishangilia baada ya kufunga bao pekee la Manchester United Uwanja wa Old Trafford
Angalia maujuzi: Hernandez akienda hewani kuunganisha kona ya Wayne Rooney
... Hernandez alivyofunga
Hiyo babu kubwa: David Moyes akishangilia bao la Hernandez
Amerudi: Luis Suarez akionekana mwenye furaha kuwa kikosini Liverpool tena
Suarez akipeana mikono na Wayne Rooney kabla ya mechi
Suarez alikaribia kufunga kipindi cha kwanza, lakini kipa wa United, David De Gea akaokoa
Suarez akipiga kichwa huku beki wa kushoto wa United, Alex Buttner akimuangalia
Yalaa: Beki wa United, Phil Jones akimchezea rafu Suarez
Gwiji wa United, Roy Keane alikuwa jukwaani akiangalia mechi
Rooney akipambana na Mamadou Sakho