IMEWEKWA SEPTEMBA 17, 2013 SAA 2:16 ASUBUHI
KOCHA David Moyes yuko hatarini kumpoteza kinda Adnan Januzaj mbele ya wapinzani, Manchester City wanaomtaka.
Kiungo huyo mwenye kipaji amekuwa kwenye utata wa Mkataba na Manchester United karibu miezi sita sasa.
City imekaa mkao wa kula katika kuwania saini ya mchezaji huyo wa Old Trafford, baada ya kuonekana kama wanashindwa kufikia mwafaka.
Mkali: Adnan Januzaj (kulia) alicheza vizuri dhidi ya Crystal Palace akitokea benchi
Wachezaji waliochezea timu zote Manchester United na Manchester City tangu Vita Kuu ya pili ya Dunia:
Denis Law, Brian Kidd, Wyn Davies, Sammy McIlroy,Peter Barnes, John Gidman, Peter Beardsley, MarkRobins, Andrei Kanchelskis, Peter Schmeichel, TerryCooke, Andy Cole, Carlos Tevez, Owen Hargreaves
Januzaj alionyesha ni mkali baada ya kutokea benchi kipindi cha pili katika mechi na Crystal Palace Jumamosi na kuisaidia United kushinda 2-0.
Pia aliingia katika mchezo wa ngao ya Jamii mwishoni mwa mwezi uliopita na kuisaidia timu kushinda.
Lakini mustakabali wake Old Trafford unaweza kuwa mfupi, vinginevyo, kocha Moyes ampe mshahara wa hadhi ya timu ya kwanza ndipo atabaki.
Januzaj, mwenye umri wa miaka 18, anamaliza Mkataba wake mwishoni mwa msimu na hadi sasa amegoma kusaini Mkataba mpya, licha ya majadiliano kuanza tangu Aprili.
Kengele za hatari zimeanza kulia juu ya Mbelgiji huyo, baada ya sasa kuanza kuomba kutolewa kwa mkopo kufuatia klabu ya Blackburn kuonyesha nia ya kumtaka.
Tumaini: David Moyes (kulia) anataka kumbakiza kinda huyo wa Manchester United, anayetarajiwa kuwa tishio baadaye