IMEWEKWA SEPTEMBA 28, 2013 SAA 3:53 USIKU
MABAO ya Leandro Bacuna na Andreas Weimann kipindi cha pili yameisaidia Aston Villa kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester City katika Ligi Kuu ya England.
Wenyeji walisota kusawazisha mara mbili baada ya Yaya Toure dakika ya 45 na Edin Dzeko dakika ya 55 kuifungia City, kwanza kupitia kwa Karim El Ahamdi aloyesawazisha la kwanza Uwanja wa Villa Park dakika ya 51.
Baadaye Bacuna akasawazisha tena kwa mpira wa adhabu dakika ya 73 na Weimann akafunga la ushindi dakika ya 76.
Kikosi cha Villa kilikuwa: Aston Villa: Guzan, Bacuna, Vlaar, Baker, Clark, Luna, Delph, El Ahmadi, Sylla 5, Weimann/Bowery dk79 na Kozak.
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Milner, Toure, Fernandinho, Nasri/Navas dk66, Negredo na Dzeko/Joevetic dk74.
Saluti: Andreas Weimann akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi
La kwanza: Yaya Toure akiifungia Manchester City
Hasira: Samir Nasri akizozana na marefa huku wachezaji wenzake wakimzuia