IMEWEKWA SEPTEMBA 21, 2013 SAA 3:24 USIKU
BAO pekee la Dejan Lovren limeipa Southampton ushindi wa 1-0 Uwanja wa Anfield dhidi ya wenyeji Liverpool leo.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Croatia alifunga bao hilo dakika ya 54 na kumaliza rekodi ya Liverpool kutofungwa ndani ya mechi 12.
Mshambuliaji Luis Suarez, alikuwepo jukwaani akishuhudia mechi yake hiyo ya mwisho katika adhabu ya kufungiwa mechi 10 na sasa anarejea uwanjani.
Pamoja na hayo The Saints, inabidi wamshukuru refa Neil Swarbrick aliyewanyima Liverpool penalti baada ya beki wao kumuangusha Daniel Sturridge kwenye eneo la hari kipindi cha kwanza.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet, Toure, Skrtel/Alberto dk72, Agger/Enrique dk56, Sakho, Gerrard, Lucas, Henderson, Aspas/Sterling dk46, Moses na Sturridge.
Southampton: Boruc, Clyne, Lovren/Fonte, Shaw, Wanyama, Schneiderlin, Rodriguez/Cork dk89, Lallana/Ward-Prowse dk75, Osvaldo, Lambert/Davis dk61.
Bao la ushindi: Dejan Lovren amfunga bao pekee la ushindi dhidi ya Liverpool
Amepatia: Wachezaji wa Liverpool wakiangalia mpira uliopigwa kwa kichwa na Lovren ukitinga nyavuni
Babu kubwa: Lovren akishangilia mbele ya mashabiki wa Southampton
Amekosa: Daniel Sturridge aisikitika baada ya kupoteza nafasi ya kufunga
Hasira: Brendan Rodgers na Steven Gerrard wakionyesha hasira zao za kufungwa
Kifaa: Victor Moses akiichezea Liverpool kwa mara ya kwanza Uwanja wa Anfield
Jino kwa jino: Kolo Toure na James Rodriguez wakigombea mpira
Mkwaju: Steven Gerrard akipiga mpira wa adhabu
Vita: Mamadou Sakho na Nathaniel Clyne wakigombea mpira
Anatazama: Luis Suarez akiangalia mechi Anfield
Mchuano: Adam Lallana akipambana na Steven Gerrard