IMEWEKWA SEPTEMBA 26, 2013 SAA 10:43 JIONI
MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski hatimaye amethibitisha atasaini kama mchezaji huru kujiunga na wapinzani, Bayern Munich ifikapo Januari na kuhamia Bavaria Mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.
Baada ya tetesi kadhaa miezi ya majira ya joto, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka 25 ataungana na kabi ya Pep Guardiola, Lewandowski ameacha Mkataba wake umalizike na ataruhusiwa kusaini Mkataba wa awali kujifunga Allianz Arena mwaka 2014.
Kwa mara ya kwanza tangu azuiliwe na kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp aliyegoma kuwauzia silaha yake wapinzani wake wa Bundesliga, Lewandowski amesema atajiunga na Munich kama mchezaji huru.
Anaondoka: Robert Lewandowski amethibitisha kuondoka Borussia Dortmund kuhamia Bayern Munich mwakani
Akijibu swali kwamba atahamia Signal Iduna Park Januari, Lewandowski alisema: "Ndiyo, kwa sababu baadaye nitasaini Mkataba rasmi,"
Njia iko wazi kwa Lewandowski kujiunga na mabingwa hao wa Ulaya baada ya kocha wa zamani wa Barcelona, Guardiola kumruhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Mario Gomez kutimkia Fiorentina, na kutoa nafasi kwa mshambuliaji mwingine.
Mtambo wa mabao: Lewandowski amefunga mabao manne Dortmund katika mechi sita za Bundesliga msimu huu
Dole: Kocha wa Bayern, Pep Guardiola amemruhusu Mario Gomez kuondoka, na kutoa nafasi ya Lewandowski kutua
Kuondoka kwa Lewandowski kutaacha pigo katika safu ya ushambuliaji ya Dortmund – ambako amefunga mabao 58 katika mechi 103 tangu ajiunge nayo mwaka 2010 kutoka Lech Poznan ya Poland.
Mwaka jana alifunga mabao 36 katika mashindano yote pamoja na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne katika Nusu Fainali moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu yake ikishinda 4-1 dhidi ya Real Madrid, kabla ya kufungwa na Bayern 2-1 katika Fainali, Uwanja wa Wembley, Mei mwaka huu.
Licha ya Munich kununua zaidi wachezaji bora na wa bei kubwa, bado timu zote zimefungana kileleni mwa Bundesliga baada ya mechi sita, kila timu ikiwa na pointi 16 na kutofautiana kwa wastani wa mabao tu ya kufunga na kufungwa