IMEWEKWA SEPTEMBA 15, 2013 SAA 7:17 USIKU
MABAO 203 katika mechi 203 kwa Cristiano Ronaldo; moja katika mchezo mmoja kwa Gareth Bale.
Hiyo ndiyo ilikuwa mwanzo wa faida za kutoa Euro Milioni 100 kumsajili mchezaji huyo baada ya Bale kufunga bao lake la kwanza Real Madrid usiku huu katika sare ya 2-2 dhidi ya Villarreal.
Bale alifunga kipindi cha kwanza na Ronaldo akafunga kipindi cha pili katika mchezo huo wa La Liga.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Diego Lopez, Carvajal, Pepe, Ramos, Nacho, Illarramendi/Khedira 60, Modric, Bale/Di Maria dk60, Isco, Ronaldo na Benzema/Morata dk72.
Villareal: Asenjo, Mario, Musacchio, Dorado, Costa, Aquino, Trigueros, Bruno, Cani, Giovani, Pereira/Uche dk64.
Bale Madrid: Winga wa zamani wa Tottenham, Gareth Bale akifurahia bao lake kwanza
Mwanzo mzuri: Bale alipewa pasi na mchezaji mwenzake mpoya, Daniel Carvajal
Cristiano Ronaldo naye amefunga
Get used to it: Bale and Cristiano Ronaldo lined up for the first time on the same team