// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); FARAJA ARSENAL, TENA FARAJA SANA TU...GIROUD ALIYEUMIA NA SUNDERLAND JUZI YUKO FITI KUCHEZA UFARANSA JUMATANO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE FARAJA ARSENAL, TENA FARAJA SANA TU...GIROUD ALIYEUMIA NA SUNDERLAND JUZI YUKO FITI KUCHEZA UFARANSA JUMATANO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 16, 2013

    FARAJA ARSENAL, TENA FARAJA SANA TU...GIROUD ALIYEUMIA NA SUNDERLAND JUZI YUKO FITI KUCHEZA UFARANSA JUMATANO

    IMEWEKWA SEPTEMBA 16, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
    MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Olivier Giroud amepunguza hofu juu ya majeruhi aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Sunderland juzi.
    Mshambuliaji huyo alitolewa nje mwishoni mwa mchezo na Arsene Wenger akasema ana wasiwasi wa kumkosa mpachika mabao huyo kikosini mwake.
    Lakini Mfaransa huyo, ambaye amefunga mabao katika kila mechi ya ligi hadi sasa, amesema atakuwa fiti kuichezea The Gunners katika mchezo mkali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano dhidi ya Marseille.
    I'm ok: There were fears that the injury Olivier Giroud picked up at Sunderland would sideline him
    Niko sawa: Kulikuwa kuna hofu kwamba maumivu aliyoyapata Olivier Giroud dhidi ya Sunderland yatamuweka nje
    Lack of depth: Arsene Wenger was worried he would be out of strikers for the game on Wednesday
    Hofu imepungua: Arsene Wenger alikuwa ana wasiwasi wa kukosa washambuliaji Jumatano

    Santi Cazorla anatakiwa kuwa nje hadi katikati ya Oktoba na alipoulizwa juu ya maumivu yake, Giroud alisema: "Si mbaya hakika, si mbaya kama nilivyohofia awali. Nilipata pigo mapema mchezoni, lakini hakuna aliyekuwa karibu yangu wakati naumia wakati huo,"alisema.
    "Nilikuwa nawania mpira nikadondokea mguu. Nikaumia kifundo cha mguu, lakini bahati nzuri, hakuna maumivu makubwa. Nipo vizuri, kweli nitakuwa safi (kwa mechi na Marseille),".
    Giroud anatakiwa kutambua ukweli kwamba alisajiliwa baada ya kuondoka kwa Robin van Persie Emirates msimu uliopita, na kiwango chake kinaenda kikikua tangu msimu uliopita.
    Ameanza vizuri msimu huu na kuna matumaini atafanya vizuri zaidi hasa baada ya kusajiliwa kwa kiungo Mjerumani, Mesut Ozil kwa dau la Pauni Milioni 42.5 kutoka Real Madrid.
    On fire: Giroud has scored in every Premier League game this season
    Na moto: Giroud amefunga bao katika kila mechi ya Ligi Kuu England msimu huu
    Assist master: But he says his job is made easier by players such as Mesut Ozil (right) setting him up
    Mtaalamu wa pasi za mabao: Lakini amesema kazi yake inakuwa rahisi zaidi kutokana na wachezaji kama Mesut Ozil (kulia) kumpa pasi za mabao

    "Huu ni mwendo mzuri ninaokwenda nao tangu nimejiunga na Arsenal na ninafikiri kinaweza kuwa kiwango kizuri zaidi.
    Na sasa tuna mchezaji wetu mpya, itakuwa nzuri zaidi.
    "Wote tulijua juu ya ubora wake (Ozil), lakini unapokuwa unacheza naye uwanjani ni nzuri sana.
    "Wakati wote anatazama nafasi na anafanya mambo haraka anapoona mwanya, ni rahisi sana. Unaweza kuona mapema ataifanya hii timu kuwa bora. Lakini ngoja tuone, kwa ubora wake, anaweza kufanya timu yoyote duniani iwe bora.
    "Sasa kila mshambuliaji ana bahati ya kutosha kuwa na wachezaji kama Ozil, Aaron (Ramsey), Jack (Wilshere), Theo (Walcott) na (Santi) Cazorla nyuma yake. Nahisi bahati sana,".
    Arsenal inakwenda Stade Veledrome kumenyana na Marseille ikihitaji matokeo mazuri katika kundi lake ambalo lina timu pia za Napoli na Dortmund.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: FARAJA ARSENAL, TENA FARAJA SANA TU...GIROUD ALIYEUMIA NA SUNDERLAND JUZI YUKO FITI KUCHEZA UFARANSA JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top