Ghana kumenyana na Misri ambayo inatrisha
TIMU ya taifa ya Ghana itamenyana na Misri katika mechi ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la mwakani nchini Braziil.
Misri ni timu pekee barani yenye rekodi ya ushindi wa asilia 100 katika mechi za kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwakani.
Mabingwa wa Afrika, Nigeria watamenyana na timu dhaifu kutoka Afrika Mashariki, Ethiopia, wakati timu bora Afrika kwa sasa, Ivory Coast watamenyana na Senegal.
Tunisia, iliyofuzu baada ya Cape Verde kupokonywa pointi, itamenyana na Cameroon.
Na Burkina Faso,washindi wa pili wa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2013, watamenyana na Algeria.
Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Oktoba 11 na 15 na za marudiano zitapigwa kati ya Novemba 15 na 19.
Timu tano zitakazoshinda baada ya matokeo ya jumla, maana yake zitakuwa zimejikatia tiketi ya kwenda Brazil mwakani.
Timu tano zitakazoshinda baada ya matokeo ya jumla, maana yake zitakuwa zimejikatia tiketi ya kwenda Brazil mwakani.